Home
»
habarizakitaifa
» MAHAKAMA YA TANZANIA YATOA MAFUNZO YA NJIA ZA KISASA/KIELEKTRONIKI ZA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KWA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU NA MAAFISA TEHAMA
Na Mary Gwera, Mahakama
Mahakama ya Tanzania
inakusudia kuendelea kuboresha utunzaji kumbukumbu kwa njia ya kiielektroniki
ili kurahisisha huduma ya utoaji haki nchini.
Hayo yalisemwa mapema jana na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Mhe.
Jaji Dkt. Paul Kihwelo alipokuwa akifungua mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu
kwa njia za Kisasa “Training on Modern Record Keeping and Document Management”
yanayoshirikisha Wasaidizi wa Kumbukumbu/Makarani kutoka Mahakama mbalimbali
nchini pamoja na Maafisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania.
“Lengo la mafunzo haya
ni kuwajengea uelewa zaidi juu ya utunzaji sahihi wa kumbukumbu za Kimahakama
ikiwemo kutumia njia za Kiielektroniki (TEHAMA) ili kurahisisha uendeshaji wa
shughuli mbalimbali za Mahakama na hatimaye kufikia lengo la uboreshaji wa
huduma ya utoaji haki kwa wananchi na umma kwa ujumla” alisema Mkuu huyo wa
Chuo.
Aliongeza kuwa katika
Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha kada mbili tofauti ya Wasaidizi wa
Kumbukumbu na Maafisa TEHAMA, ni kuwawezesha kuwa kitu kimoja kwakuwa wao ndio
watakaotengeneza na kutumia mifumo hiyo.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi Msaidizi-Mafunzo, Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu
alisema mafunzo haya ambayo yameshirikisha jumla ya Washiriki 51 yanalenga
katika kuwajengea uwezo juu ya utunzaji wa kisasa wa kumbukumbu.
Aliongeza kuwa mafunzo
hayo yameshirikisha Washiriki kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, Arusha,
Manyara, Bukoba, Divisheni zote za Mahakama Kuu ambazo ni Divisheni ya
Biashara, Kazi, Ardhi na Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kibaha, Morogoro, Dodoma,
Iringa, Njombe, Songwe, Sumbawanga, Shinyanga na Simiyu.
Aidha; Bi. Ngungulu
alisema kuwa, baada ya mafunzo hayo ya siku 10 yanayofanyika chini ya ufadhili
wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama chini ya Benki ya Dunia ‘WB’ wanatarajia
kuona wahitimu hao wanaboresha utunzaji sahihi wa kumbukumbu katika maeneo yao
ya kazi na pia kutoa ujuzi kwa wale ambao hawakushiriki ili kuwa na uelewa wa
pamoja.
Mafunzo haya ni muendelezo
wa mafunzo kwa Wasaidizi wa kumbukumbu (RMAs) yaliyokwishafanyika mkoani Dodoma
chini ya Mradi wa Mapambano dhidi ya Rushwa ‘STACA,’ ambapo kwa sasa mafunzo
haya yatatilia mkazo juu ya utunzaji wa kisasa wa nyaraka na kumbukumbu za
Mahakama ikiwemo matumizi ya vitendo vya kutumia mfumo wa Kielektroniki katika
kutunza na kushughulikia kumbukumbu hizo kwa ujumla.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama-IJA-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo akifungua rasmi Mafunzo ya
Utunzaji wa Kumbukumbu kwa njia za kisasa “Training on Modern Record Keeping
and Document Management” yanayoshirikisha Wasaidizi wa Kumbukumbu na Maafisa
TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala, Bw. Edward
Nkembo.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA-
Lushoto alipokuwa akifungua mafunzo hayo ya siku yanayofanyika katika chuo
hicho kilichopo mkoani Tanga.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA-
Lushoto alipokuwa akifungua mafunzo hayo ya siku yanayofanyika katika chuo
hicho kilichopo mkoani Tanga.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA-
Lushoto alipokuwa akifungua mafunzo hayo ya siku yanayofanyika katika chuo
hicho kilichopo mkoani Tanga.
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Mhe. Jaji. Dkt. Paul Kihwelo, (wa pili kulia),
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward
Nkembo (wa pili kushoto), Mkurugenzi-Msaidizi-Mafunzo, Mahakama ya Tanzania,
Bi. Patricia Ngungulu, wa kwanza kushoto na Mratibu wa Mafunzo ya Mahakama
toka Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA,
Bw. Lameck Samson (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Maafisa TEHAMA na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanaoshiriki katika mafunzo hayo.
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Mhe. Jaji. Dkt. Paul Kihwelo, (wa pili kulia),
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward
Nkembo (wa pili kushoto), Mkurugenzi-Msaidizi-Mafunzo, Mahakama ya Tanzania,
Bi. Patricia Ngungulu, wa kwanza kushoto na Mratibu wa Mafunzo ya Mahakama
toka Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA,
Bw. Lameck Samson (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Maafisa TEHAMA na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanaoshiriki katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu- Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward akieleza jambo
kwa washiriki wa Mafunzo.
Baadhi
ya washiriki wa Mafunzo
Baadhi
ya washiriki wa Mafunzo
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- Zanzibar to Organize a Half Marathon race to Promote Gender Mainstreaming, Attain Sustainable Development Goal06 Jan 20180
More than 300 Zanzibari women, men, girls and boys are expected to participate in t...Read more »
- Embassy of Kuwait in Tanzania Committed to Support Educational Projects in Zanzibar18 Dec 20170
Member of the House of Representative in Zanzibar, Hon Simai Mohammed Said in discussion ...Read more »
- Turkey to intensify relationship with SUZA16 Aug 20170
Delegation of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) meets Prof. Rai (...Read more »
- RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WATEMBELEA KUWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM28 May 20170
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamo...Read more »
- Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini18 May 20170
Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kucha...Read more »
- NAIBU MKURUGENZI WA IMF AKUNWA NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, AAHIDI KUFUNGUA DIRISHA LA MIKOPO KWA TANZANIA18 May 20170
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kulia) akiel...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.