 |
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea wakati wa mahafali
ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto
waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga |
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga
amekemea vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike nchini na kuahidi
kuwachukulia hatua kali za kisheria wale watakaobainika.
Akiongea
wakati wa Mahafali ya watoto 46 waliokimbia kukeketwa na kujiunga na
Kituo cha kulea watoto hao cha ATFGM Kilichopo Masanga Tarime Vijijini
Bi.Sihaba alisema kuwa suala la ukeketaji ni kinyume na sheria za nchi
na haki za binadamu na ni suala lenye madhara kwa maisha ya watoto.
“Hatukubaliani
na suala hili kwani linarudisha maendeleo ya nchi yetu,suala hili pia
linachangia kurudisha fikra za vijana wetu na kubatilisha ndoto za
vijana wetu, tunao muda wa kujirekebisha na kama tulikuwa tunaendelea
basi turudi nyuma”Alisema Bi. Sihaba.
Katibu
Mkuu huyo amesema kuwa jamii inayo wajibu wa kulinda na kuendeleza mila
zenye kuleta maendeleo na kuacha kulinda na kukumbatia mila
zinathoathiri maisha ya binadamu kwani sio suala sahihi kwani mila
nyingine zinagharimu maisha ya vijana wetu.
Akizungumza
katika mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Glorious Luoga
amewakemea wazazi watakaothubutu kuwakeketa wasichana wanaotoka katika
kituo hicho baada ya mafunzo na wale watakao watakaowatahiri watoto wa
kiume kwa mara ya pili baada ya kufanyiwa tohara salama hospitalini.
“Niwaeleze
wazazi na walezi, wapo wanaowalazimisha kuwafanyia tohara ya pili
watoto wa kiume baada ya kufanyiwa tohara salama, atakayegundulika
kufanya tukio hilo tutamshughulikia kwa kumchukulia hatua kali za
kisheria ili aone uchungu anaoupata mtoto wakati wanawatahiri kwa mara
ya pili” Alisema Mhe. Luoga.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi. Lydia Bupilipili amewasihi wazazi kuacha
tabia ya ukeketaji na kuwapeleka watoto shule ili waweze kutimiza
malengo yao kwani kila mtoto ana talanta aliyopangiwa na mungu hivyo
kufanya hivyo kuwakeketa na kuwazuia kwenda shule ni kukatisha malengo
yao.
Mkurugenzi
wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga)
Sister Stella Mgaya ameshukuru juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na
uongozi wa wilaya ya Tarime kukabiliana na tatizo hilo na kuendelea
kuomba wadau kujitokeza kuwaendeleza watoto wanaohitimu kituoni hapo.
“Tunashukuru
jitihada za Wilaya ya Tarime wamekuwa nasi bega kwa bega ila tunaomba
wadau wengine ikiwemo serikali kwani baada ya mafunzo watoto hawa
wamekuwa wakitengwa na familia zao na kuacha kuwapa mahitaji ya msingi
hivyo kulazimu kituo kugharamia masomo japo sio kwa kiwango cha
kuridhisha” Alisema Sister Mgaya.
Wakisoma
Risala kwa mgeni rasmi muwakilishi wa wahitimu hao Magreth Daniel
ameiomba serikali kuendelea kuwasaidia hasa baada ya mafunzo na kuepuka
kutengwa na familia pia kuendelea kuwachukulia hatua za kisheria
wazazi,walezi na mangariba wanaojishughulisha na vitendo vya ukeketaji.
Kituo
cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga kwa mwaka
jana kimepokea watoto 300 kutoka katika maeneo ya Tarime,Rorya,Bunda,
Loliondo na baadhi kutoka nchi jirani ya Kenya.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.