Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: West Ham wawasogezea Chelsea ubingwa.
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Sasa ni mechi mbili tu zimebaki ili Chelsea kutawazwa kuwa mabingwa baada ya Tottenham hapo jana kukubali kipigo cha bao moja kwa sifuri...
Sasa ni mechi mbili tu zimebaki ili Chelsea kutawazwa kuwa mabingwa baada ya Tottenham hapo jana kukubali kipigo cha bao moja kwa sifuri toka kwa West Ham.
Kabla ya mchezo huo kocha wa West Ham Slaven Bilic alionywa na wamiliki wa timu hiyo kuhusu kupoteza mchezo huo, Bilic angekubali kufungwa kibarua chake kingekuwa mashakani na hivyo kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa Tot.
Alikuwa Manuel Lanzini dakika ya 65 ndio ambae aliisimamisha Tottenham katika mbio zao za kuifukuza Chelsea ambapo sasa Westham inaungana na Manchester United,Liverpool na Chelsea kama timu zilizoifunga Tottenham msimu huu.
Chelsea wenyewe ambao wanahitaji alama 6 tu ili kuwa mabingwa, watakuwa uwanjani siku ya Jumatatu kuwakaribisha Middlesbrough katika uwanja wao wa nyumbani ambapo wakishinda mchezo huo watabakisha mchezo mmoja tu.
Leo kuna mechi zitaendelea kupigwa ambapo itakuwa kati ya Man City vs Crystal Palace, Bournaouth vs Stoke City, Hull City vs Sunderland, Burnley vs West Bromich, Leicester vs Watford na Swansea vs Everton.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top