Cristiano Ronaldo anatajwa kama mfalme wa Champions League
kutokana na mambo anayoyafanya katika mashindano hayo, lakini upande wa
pili wa Lioneil Messi hawakubali hili wakidai nyota wao ni bora kuliko
Mreno, leo tuone baadhi ya ubora kati ya nyota hawa wawili.
Mabao. Wanasema mpira ni magoli sasa Cristiano Ronaldo anaongoza
katika ufungaji katika mashindano hayo, hadi sasa ana mabao 103 ambayo
ameyafunga katika michezo 138, ambapo mashabiki wa Lioneil Messi
wanakataa kusema Ronaldo anafunga kuliko Messi kwani Lioneil Messi ana
mabao 94 ambayo kayafunga katika michezo 115 ambayo ni michezo 23
pungufu ya Ronaldo, wanaamini Messi angecheza michezo sawa na Ronaldo
angefunga mabao zaidi ya 103 hadi sasa.
Wastani wa dakika kwa kila bao. Mabao ambayo Cristiano ameyafunga
hadi sasa ni 103 lakini inaonekana Mreno huyo anatumia mda mrefu sana
kufunga kuliko Lioneil Messi kwani Ronaldo huwa inamchukua dakika 116
kufunga bao moja wakati Lioneil Messi yeye huwa inamchukua dakika 101 tu
kufunga bao moja.
Jinsi walivyofunga mabao yao. Mashabiki wa Messi wameibuka na jina la
utani wakimuita Ronaldo “Penaldo” wakimaanisha anafunga magoli mengi ya
penati na jedwari la ufungaji wao linaonesha Cristiano Ronaldo magoli
yake 22.3% ameyafunga kupitia freekicks na penati huku 77.3% akifunga
kawaida, lakini Lioneil Messi amefunga mabao yake 13.8%tu amefunga kwa
freekick na penati huku 86.2% akifunga kawaida.
Assists. Ronaldo anaonekana ana mchango mkubwa kwa Real Madrid katika
assists kwani katika michezo aliyocheza kila baada ya dakika 362 alitoa
assist huku Lioneil Messi akichukua mda mrefu kidogo kutoa assist kwani
ametumia mda mrefu kidogo kutoa assists kwani ametumia dakika 381 kutoa
assists.
Misimu waliyoibuka vinara wa ufungaji. Hapa pia Ronaldo na Lioneil
Messi wako sawa ambapo wote hadi sasa wamekuwa wafungaji bora wa UCL
kila mmoja kwa misimu mitano, kiujumla nyota hawa wote wanaonekana ni
bora katika michuano hii japokuwa Cristiano Ronaldo anaonekana bora
zaidi msimu huu ila Messi kwa upande mwingine anaonekana bora sana.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment