Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Christian Eriksen
amekuwa na msimu mzuri sana safari hii, mchango wake mkubwa ndani ya
klabu hiyo umeifanya Tottenham kuwa mshindani mkubwa katika mbio za
ubingwa.
Japokuwa katika kikosi cha Tottenham jina lake limekuwa halitajwi
sana kama wanavyoongelewa Delle Ali na Harry Kane lakini mchango wa
kiungo huyu ni mkubwa sana na pengine ndio unaomfanya Kane aonekane bora
kila kukicha
Eriksen sasa ameingia katika vitabu vya rekodi vya ligi kuu nchini
Uingereza baada ya kiungo huyo kuwa kiungo wa kwanza katika msimu huu wa
ligi kutengeneza nafasi zaidi ya 100 za ufungaji hadi sasa.
Katika takwimu zilizofanya na shirika moja la masuala ya michezo
inaonesha msimu huu hakuna kiungo aliyetengeneza nafasi 100 wakati
Eriksen pekeyake amevuka 100 sasa ana 101 na kati ya hizo 12 zilileta
magoli.
Katika orodha hiyo kiungo wa Manchester City Kelvin De Bruyne yuko
katika nafasi ya pili akiwa ametengeneza nafasi 90 akifuatiwa na Ross
Barkley wa Everton ambaye ametengeneza nafasi 80.
Kama hiyo haitoshi Eriksen yupo katika orodha ya wachezaji wawili wa
juu katika Epl wanaoongoza kwa kutoa assits ambapo jina lake liko nafasi
ya pili chini ya kiungo wa Manchester City Kelvin De Bruyne.
Msimu huu hadi sasa Eriksen ametoa assists 12 wakati De Bruyne akiwa
kileleni na assist moja zaidi kwa Eriksen, nafasi ya tatu yuko kiungo wa
klabu ya Swansea Gylfi Sigurdson ambaye ana assists 12.
Mchango wa Eriksen hadi sasa umeifanikisha Tottenham kuwa nafasi ya
pili na alama zao 77 zikiwa zimebaki mechi 4 kwa ligi kumalizika huku
vinara Chelsea wakiwa kileleni na alama zao 81.
Kiungo wa Tottenham Hotspur aweka rekodi Epl. Inbox x
Title: Kiungo wa Tottenham Hotspur aweka rekodi Epl. Inbox x
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Christian Eriksen amekuwa na msimu mzuri sana safari hii, mchango wake mkubwa ndani ya klabu hiyo u...
Post a Comment