Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Ushindi wa Madrid wazua mapya nje ya uwanja
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Washindi mara 11, Real Madrid wamefika hatua ya fainali mara mbili mfululizo kuliko klabu nyingine yoyote ya soka barani ulaya, hivyo kuwa...
Washindi mara 11, Real Madrid wamefika hatua ya fainali mara mbili mfululizo kuliko klabu nyingine yoyote ya soka barani ulaya, hivyo kuwa shangaza wengi kuwa klabu ya kwanza kutetea Ubingwa huo na kufanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya Champions League


mfungaji wa goli la Real Madrid akionekana kuwa kejeli wapinzani wao.
Katika hatua ya robo fainali, imeonekana kuwa rahisi kwa klabu hiyo ilipokutana na klabu ya Bayern Munich, kuliko ilivyotarajiwa licha ya mabao mawili ya utata yaliyopatikana katika mchezo wa marudiano, mchezo uliofanyika nchini Hispania. Na mchezo wa Madrid Derby ulikuwa mwepesi pia kwao baada ya nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kufunga magoli matatu na kukifanya kikosi cha Zidane kuwa na kazi rahisi katika mchezo wa marudiano.


Christian Ronaldo akiupaka mafuta Mpira mbele ya Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simion .
Kwa ushindi wa Mabingwa wa Italia, kibibi cha Turin, klabu ya Juventus,wa jumla ya mabao 4 kwa 1 dhidi ya klabu ya Monaco unawafanya kushindania taji la Champions Leegue tangu walivyo fanya hivyo miaka 21 iliyopita.


Kikosi cha Real Madrid kikishangilia kutinga hatua ya Fainali ya Champions League.
Klabu ya Real Madrid dhidi ya Juventus katika mchezo wa fainali hii ya Uefa Champions League inawarudisha nyuma hadi mwaka 1998 ambapo walikutana katika fainali kama hii na Madrid kutwaa ubingwa kwa goli la mchezaji wake Predrag Mijatovic’s.

Kikosi cha Madrid kilichotwaa ubingwa mwaka 1998 mbele ya Juventus, watakaokutana tena mwaka huu.
Kocha wa Madrid Zinedine Zidane akumbuka alivyo ichezea Juventus enzi zake.
Mchezo huu unamaana kubwa kwa Meneja wa Real Madrid Zidane, ambae aliwahi kucheza fainali hizi akiwa upande wa klabu ya Italia.

Kocha wa Real Madrid, Zidane alipo ichezea Juventus miaka ya 1996 na 2001.
“Imekuwa klabu muhimu sana kwa upande wa taaluma na naichukulia hii kama klabu ambayo niliiatia kila kitu nilicho stahili kukifanyal,” alisema Mfaransa huyo ambae amewahi kuihudumia klabu ya Juventus kati ya mwaka 1996 na 2001.


Mashabiki waking’oa viti kujikinga na mvua, wakionyesha furaha zao bila kujali.
Maneno ya Zidane baada ya Ushindi dhidi ya Atletical Madrid
“Tuna furaha kuingia hatua ya fainali, na furaha zaidi kuingia fainali kwa mara ya pili mfululizo. Tulistahili, hasa kwa wachezaji ambao wamefanya kazi kubwa mpaka sasa. Tunastahili.

“Tulikuwa katika wakati Mgumu sana mwanz wa safari yetu. Tulipata magoli mawili pekee, Lakini hatukujali. Tulijua kuwa tutakuwa na nafasi.
“Tulijua watakuja na nguvu mpya, pamoja na presha. Lakini baada ya ya dakika 25 kila kitu kilibadilika. Katika kipindi cha pili, tukarudi mchezoni.” Alisema Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane.
Maneno ya wachezaji wa Real Madrid baada ya ushindi.

Christian Ronaldo katika mtandao wake wa Twitter.

Maneno ya Beki wa Real Madrid Marcelo kupitia twitter

Karim Benzema Mchezaji wa Real Madrid.

Gareth Bale wa Real Madrid kupitia Twitter.
Yalioandikwa katika mitandao ya michezo ulaya.








HAYO NDIO YALIO JIRI NDANI YA UWANJA NA NJE YA UWANJA,

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top