Katika mechi saba (7) zilizopita za hivi karibuni za ligi kuu
Tanzania bara, Tanzania Prisons haijashinda hata mechi moja dhidi ya
Yanga, imefungwa mechi tano na kutoka sare mara mbili ikicheza na Yanga,
hiyo inatosha kutoa picha ya namna ambavyo Prisons wamekuwa
wakinyanyaswa na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara.
19/09/2013 Tanzania Prisons 1-1 Yanga
26/03/2014 Yanga 5-0 Tanzania Prisons
28/09/2014 Yanga 2-1 Tanzania Prisons
18/02/2015 Tanzania Prisons 0-3 Yanga
16/09/2015 Yanga 3-0 Tanzania Prisons
03/02/2016 Tanzania Prisons 2-2 Yanga
06/11/2016 Tanzania Prisons 0-1 Yanga
06/05/2017 Yanga ?? Tanzania Prisons
Mchezo wa Azam Sports Federation Cup uliopigwa April 22, 2017 bado
Yanga waliendeleza manyanyaso kwa maafande hao wa jeshi la Magereza kwa
kuwanyuka bao 3-0 katika mchezo wa robo fainali na kuwatupa nje ya
mashindando kabla ya Yanga kukutana na kigingi cha Mbao kwenye nusu
fainali na kuvuliwa ubingwa kwa kufungwa kwa goli 1-0.
Mchezo wa leo Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na njaa ya matokeo
ambayo yatawafanya wawafikie watani zao Simba kwa idadi ya pointi na
Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya wastani wa magoli. Yanga ina pointi
56 ikiwa imecheza mechi 25 pointi tatu nyuma ya Simba ambayo imecheza
mechi 27 hadi sasa ikiwa na pointi 59.
Yanga ina sababu nyingi za kutaka ushindi dhidi ya Tanzania Prisons
‘iwe mvua au liwe jua’ lazima watafute ushindi na kujiweka kwenye nafasi
nzuri ya kutetea taji lao la VPL.
Michuanno ya kimataifa
Ni taji la VPL pekee ndio litawafanya Yanga wacheze michuano ya
kimataifa kwa msimu ujao, wameshaondolewa kwenye kombe la Azam Sports
Federation hivyo njia yao ya kushiriki michuano ya kimataifa imebaki
moja. Wakichukua taji la VPL inamaanisha watakuwa na uhakika wa kucheza
michuano ya vilabu bingwa Afrika, wakilikosa msimu ujao wabaki
watazamaji kwenye michuano hiyo ambayo.
Kutuliza mashabiki
Ushindi dhidi ya Tanzania Prisons utatuliza presha za mashabiki ambao
tayari presha zao zilishaanza kupanda na kushuka baada ya timu yao
kuvuliwa ubingwa wa Azam Sports Federation Cup na Mbao baada ya kuchapwa
1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali na kuliachia kombe hilo ambalo
walilitwaa msimu uliopita.
Kuweka Historia
Yanga wananjaa ya kuweka historia ya kuchukua taji la VPL kwa mara ya
tatu mfululizo, ushindi dhidi ya Prisons utatoa taswira halisi ya
ubingwa wa msimu huu kwa upande wao bila kujali matokeo ya mpinzani wao
katika mbio za ubingwa.
Timu kujiamini
Ushindi dhidi ya Prisons utawafanya wachezaji kujiamini na kuendelea
kujituma kutetea taji lao ukilinganisha na wakipoteza mechi hiyo. Kama
watapoteza mechi dhidi ya Prisons itakuwa ni mechi ya pili mfululizo
wanapoteza katika mataji mawili tofauti ambayo wanayatetea na huenda
ikaondoa hali ya kujiamini na kuongeza presha kwao juu ya mbio za
ubingwa.
Kuongoza ligi
Kama Yanga watashinda dhidi ya Tanzania Prisons watarejea kwenye
nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha alama 59 sawa na
Simba lakini mabingwa watetezi wa taji la VPL wako juu kwa wastani wa
magoli. Yanga wana wastani wa magoli 39 hadi sasa wakati Simba wakiwa na
wastani wa magoli 30.
Kisaikolojia ina faida kwa wachezaji ukizingatia watakuwa wako nyuma
ya Simba kwa mchezo mmoja, Simba wakishinda kesho dhidi ya African Lyon
watarudi kileleni kwa kufikisha pointi 62, wakitoka sare watafikisha
pointi 60 lakini endapo watapoteza mchezo wao watasalia katika nafasi ya
pili na hapo ndipo Yanga watakuwa na faida zaidi ya Simba katika mbio
za kuwania taji la VPL msimu huu.
Prisons si timu ya kubeza, ikumbukwe mnyama alikaa kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya kwa kichapo cha magoli 2-1 katika mchezo wa raundi
ya kwanza msimu huu. Kufika hatua ya robo fainali ya FA ni mafanikio kwa
upande wao ukizingatia walitolewa na timu inayotetea taji.
‘Wajelajela’ wapo katika nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi kuu Tanzania
bara wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza michezo 27 pointi sawa na
African Lyon lakini wakitofautishwa na wastani wa magoli.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment