Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: United haoo wanarudi nyumbani na goli la ugenini
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Manchester United wameendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya Europa msimu huu baada ya usiku wa jana kuibuka kidedea dhidi ya ...
Manchester United wameendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya Europa msimu huu baada ya usiku wa jana kuibuka kidedea dhidi ya Celta Vigo.
Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa kimiani na Marcus Rashfor baada ya kupiga free kick iliyoenda wavuni moja kwa moja katika dakika ya 67.
Ushindi wa Manchester United umekuja wakati muafaka hasa katika kipindi hiki ambacho hawana uhakika wa kumaliza ligi katika nafasi nne za juu na hivyo kubeba Europa ni muhimu kwao ili kushiriki Champions League msimu ujao.
Celta Vigo walionekana wagumu sana katika mchezo huo kwani walikuwa wakishambuliana kwa zamu na United huku washambuliaji wa Celta Vigo Iago Aspas na mchezaji mwenye asili ya Uganda John Guidetti wakilishambulia lango la United.
Ngome imara ya ulinzi ya United ikiongozwa na Eric Bailly aliyetoka majeruhi waliyamudu mashambulizi ya Celta Vigo na kuifanya timu yao kumaliza mechi salama.
United ambao sasa wanarudi nyumbani na faida ya goli la ugenini jinamizi la majeruhi linaonekana bado linawaandama kwani usiku wa jana Ashley Young alicheza dakika chache tu akatoka kutokana na maumivu huku Marcus Rashford nae akitoka huku anachechemea.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top