Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imezindua jukwaa la uwezeshaji
wanawake kiuchumi kwa wanawake wa Wilaya ya Handeni kwenye ukumbi wa maount Ilulu uliopo Kabuku
mjini lenye ujumbe wa “Wezesha wanawake
kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda”.
Jukwaa hili linalengo la kuwakutanisha wanawake pamoja na kujadili
fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli
nyingine za kiuchumi katika Wilaya ya Handeni.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa
Jukwaa hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Bw. John Mahali aliyekuwa mgeni rasmi
akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alisema kuwa jukwaa
la wanawake hilo litasaidia kuongeza uelewa kwa wanawake katika
upatikanaji wa mitaji , sheria za nchi
katika masuala ya kiuchumi na jinsi ya kujitegemea.
Aliongeza kuwa wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi
hapa Nchini hata na duniani kote kutokana na kutokuwa na usawa katika fursa ,
uwezo wa kupata mitaji.
“jukwaaa litasaidia kuondoa
matabaka na sheri ambazo zitasaidia kupunguza ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake,
ambalo ni jambo la muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa katika pato la
Taifa, jamii na familia” alisema Bw. John.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni
Bw. William Makufwe alisema kuwa jukwaa
hili litafanya kazi ya kutambua shughuli za kijasiliamari katika kutoa elimu
kuhusu upatikanaji wa mitaji, kusajili biashara, kuwezesha kiuchumi na kutafuta
masoko.
Aidha, alisema katika suala la utoaji mikopo vikundi vitakavyopewa
kipaumbele ni vile viliyojidhatiti kwa kusajiliwa, vyenye utawala unaoeleweka,
miradi inayoonekana na zenye hesabu za kifedha zinazoweza kukaguliwa na
kukosolewa inapobidi.
Uzinduzi huo ulipambwa na maonesho ya
bidhaa za kijasiliamari ya vikundi mbalimbali kutoka kata mbalimbali. Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga
itaratibu shughuli zote za uchumi kwenye Wilaya zote ndani ya Mkoa na
kuhakikisha kunakuwa na majukwaa ya Wilaya/Halmashauri zote ambayo
yatafanya vikao vyake kila baada ya miezi
sita (6).
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe
wakwanza kulia akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali
wakitazama Moja ya bidhaa ya vikapu vinavyotengenezwa na kikundi cha
wanawake tupendane cha segera
Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali akizungumza na wanawake waiojitokeza kwenye Uzinduzi wa jukwaa Hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji Bw William Makufwe akionesha katiba waliyopewa viongozi wa
jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya itakayowasaidia Katika
Uongozi wao
Mwenyekiti
wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi
akipokea katiba kutoka Kwa mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya Bw John
Mahali.
Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akishukuru wanawake waliompa dhamana ya kuwaongoza.
Baadhi ya vikundi vya wanawake waliojitokeza kuonesha bidhaa zao wakati wa Uzinduzi.
Baadhi ya wanawake wakishiriki wa Uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya ya Handeni
Viongozi wakipata maelezo kutoka vikundi vya kinamama.
Post a Comment