Tanga,
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawa ya
kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama
kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza
katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili
Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga
International Conference Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa
itakuwa endelevu.
Alisema
vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na
Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.
“Kuna
wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine
wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya
kulevya” alisema Shighela na kuongeza
“Ili
kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya
ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya”
alisema
Kwa
upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand,
amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama
ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na wagonjwa wa Afya ya Akili.
“Niuombe
uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika
matumizi yake kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila
ambapo kunahitajika msaada” alisema
Nae
Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na
changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa
kwenda vituo vinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.
Balozi
wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie akiongea katika hafla ya fupi
ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo
lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre
(TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela akizungumza
katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili
Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga
International Conference Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa
itakuwa endelevu.
Sehemu
ya wageni katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya
Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga

Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza
kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita
(kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo
lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre
Tanga.
Post a Comment