KIKOSI
cha timu ya Simba kimeendelea kujifua kwa nguvu wakijiandaa na mchezo
wa nusu fainali dhidi ya Azam utakaofanyika mwishioni mwa wiki hii.
Jumamosi
ya April 29, ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho la Azam
HD baina ya Simba na Azam itakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Kwa
sasa Simba wapo Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambapo chini ya
Kocha Joseph Omog na Jackson Mayanja kimeamua kujichimbia huko kwa ajili
ya kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya
mbalimbali.
Hii
inakuwa ni mechi ya ushindani mkubwa sana kwa timu hizi mbili
zikikutana kwa mara ya tatu ndani ya msimu mmoja ambapo katika michezo
miwili ya awali ila mmoja akishinda mchezo mmoja.
Kwa
mujibu wa Kiongozi wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wana ari
kubwa sana na wako vizuri na wanaamini watapigana mpaka mwisho ili
kupata ushindi kwenye mchezo huo.
"Huu
ni mchezo muhimu sana kwetu, ni muhimu kupata ushindi ili tuweze
kuingia fainali ya kombe la Shirikisho na wachezaji wana ari kubwa sana
ya ushindi na wameahidi kupambana mpaka mwisho,"amesema Ally.
Mpaka
sasa Kikosi cha Simba kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao
wanatarajiwa kuukosa mcheoz huo ambao ni Hamad Juma na Jamal Mnyate.
Wachezaji
wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao wa nusu
fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya
Azam.
Golikipa Peter Manyika akiwa katika mazoezi kulekekea mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.
Wachezaji
wa Simba wakimsikiliza Kocha Joseph Omog katika maandalizi ya mechi ya
nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi.
Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.
Post a Comment