Kamishna
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akisoma hotuba yake
wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Woman And Youth Political Participation
Enhanced In 2019 Aand 2020 General Election In Tanzania uliofanyika
kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo na kushirikisha
wadau mbalimbali kutoka ,Serikalini. Vyama vya siasa, Mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za Kiraia.
Mradi
huo utakaotekelezwa na Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA na TYC na WE
Effect huku ukifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kiasi cha sh ilingi
Bilioni 1.4na utatekelezwa kwa miaka mitatu.
Lengo
la Mradi huo ni Kuongeza Ushiriki wa wanawake na vijana kwenye
uwakilishi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019-2020 katika
ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa, Mradi huu pia
unalenga kuangalia vizuizi vinavyokwamisha wanawake na vijana kushiriki
kwenye mchakato wa kugombea uongozi wa kisiasa na kuangalia ni jinsi
gani vizuizi hivyo vinaweza kutatuliwa.
Mwakilishi
wa Jumuiya ya Ulaya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Roeland
Van De Geer akitoa ujumbe wake kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa
mradi huo, Jumuiya ya Ulaya ndiyo iliyofadhili mradi huo .
Mwenyekiti
wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa
jijini Dar es salaam.
Mama
Anna Mngwira aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mwaka 2015 na mwanachama wa Chama cha wanasheria wanawake akifuatilia
kwa makini uzinduzi wa mradi huo
Baadhi
ya waalikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia hotuba mbalimbali
zilizotolewa na viongozi wa mashirika na taasisi za serikali.
Mkurugenzi
wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile
akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Kamishna
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akikaribishwa na
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka
wakati alipowasili kwenye hoteli ya New Africa kwa ajili ya uzinduzi wa
mradi huo.
Baadhi ya maofisa kutoka TAWLA wakisimamia uasili na kuwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkurugenzi
wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile pamoja na
wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Afisa kutoka Makao Mkuu ya CCM Ofisi Ndogo ya Lumumba Bw. Suleiman Mwenda pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi.
Asina Omary akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa katika mara
baada ya uzinduzi huo.
Post a Comment