Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Mfahamu, Coyo aliyechukua nafasi ya Barakah The Prince, Tetemesha (Video)
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki Coyo amefunguka kuzungumzia ujio wake mpya akiwa chini ya label kongwe ya muziki nchini, Tetemesha Records iliyokuwa ik...


Msanii wa muziki Coyo amefunguka kuzungumzia ujio wake mpya akiwa chini ya label kongwe ya muziki nchini, Tetemesha Records iliyokuwa ikimsimamia muimbaji Barakah The Prince na kumweka kwenye ramani ya muziki kabla ya kwenda ROCKSTAR 4000.
Label hiyo imewatoa wasanii kama Barakah The Prince, Hussein Machozi, Sajna pamoja na CSir.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Coyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Ziwafikie’ amesema amejisikia furaha kufanya kazi na label hiyo huku akiwataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya kazi nyingi zaidi.
“Kuna kazi ambayo imenikutanisha na Kid ambaye ni bosi wa Tetemesha lakini kabla ya hapo mimi niliongea na Kid baada ya kuisikia kazi yangu ya ‘Noma’. Lakini mimi ni mtu ambaye nilihitaji sana msaada wake pia na yeye alikuwa ananiangalia kwa jicho lingine kwa kugundua kwamba nina uwezo na kile nilichonacho na tunaweza kukiboresha zaidi na kufika pale tunapopahitaji,” alisema Coyo.
Kuhusu wimbo wake mpya alisema “Ziwafikie ndio kazi yangu mpya sasa, ilianza kutoka video na baadaye ikaja audio lakini namshukuru mwenyezi Mungu mapokezi yamekuwa makubwa sana.”
 
Angalia video yake mpya ya wimbo ‘Ziwafikie’.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top