Nyota ya ‘Hollywood Walk of Fame’ ya Rais wa Marekani, Donald Trump iliyopo Los Angeles imeharibiwa kwa mara nyingine.
Mtu asiyejulikana ameichafua nyota hiyo kwa kuiandikia matusi yaliyoelekezwa kwa Trump ambaye, amezidi kuonekana kukutana na changamoto kubwa kwa baadhi ya watu kutomkubali kutokana na sera zake za uongozi.
Fundi akitengeneza upya nyota ya Trump iliyoharibiwa mwaka jana
Oktoba mwaka jana, nyota hiyo hiyo ilivunjwa na watu asiofahamika na hatimaye ilifanikiwa kutengenezwa tena.
Inadaiwa gharama za kutengeneza nyota hizo ni dola 30k.
Post a Comment