Usiku wa jana April 23 kulikuwa na mchezo wa El Classico, mchezo ambao ulitabiriwa kuamua bingwa wa ligi hiyo (La Liga) kutokana na endapo Real Madrid ingeshinda mchezo huo ingeweza kumshinda mpinzani wake kwa tofauti ya point 6 pamoja na mchezo mmoja mkonini, kitu ambacho ingekuwa ni vigumu kwa Barcelona kumpindua mpinzani wake huyo kileleni kutokana na michezo ambayo imebaki katika ligi hiyo.
Chachu kubwa ya ushindi wa Barcelona katika mchezo wa jana ni mshambuliaji wake machachari Leonel Messi ambaye alicheza mpira mwingi sana katika mchezo huo na kufanikiwa kuipachikia timu yake mabao mawili kati ya 3 ambayo timu hiyo ili yapata dhidi ya 2 ya Real Madrid.
Ushindi huo umeiwezesha Barcelona kukaa kileleni kwa muda huku yakisubuirwa matokeo ya mchezo mmoja wa mkononi wa Real Madrid.
Post a Comment