Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: N’golo Kante, Dele Alli wang’ara tuzo za PFA Uingereza
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea, N’golo Kante, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England ...
Kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea, N’golo Kante, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA kwa msimu wa 2016-17.

N’golo Kante
Kante amewapiku nyota wengine wa ligi hiyo Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez waliokua wakiwani tuzo hiyo pia.
Kiungo wa Tottenham Dele Alli, ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mwaka wa pili mfululizo, na kuwapiku Michael Keane wa Burnley, Romelu Lukaku, kipa wa Sunderland Jordan Pickford na Leroy Sane wa Manchester City walikua wakiwani tuzo hiyo ya mchezaji chipukizi wa mwaka.
Lucy Bronze wa Manchester City ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka katika hizo, huku Jess Carter anayechezea Birmingham ameibuka kidedea kwa kuwa chipukizi bora kwa upande wa wanawake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top