Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha
sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano
Aprili 26, 2017.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.
“Nipende
kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia
mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri
Mhagama.
Amesema
sherehe hizo zitakuwa na upekee wa aina yake ukizingatia kuwa ni mara
ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
Akitaja
upekee huo, Waziri Mhagama amesema sherehe hizo zitapambwa na Gwaride
la heshima lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Maonesho ya
Kikosi cha Makomando, Onesho la Mbwa na Farasi waliofunzwa, onesho la
Ukakamavu la Uzalendo la Wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Dodoma,
burudani za vikundi vya ngoma kutoka Kaskazini Pemba pamoja na Bendi ya
mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma, Yamoto Bend na Mwenge Jazz.
“Ikumbukwe
hii itakuwa mara ya kwanza kuiadhimisha sherehe hii ya Miaka 53 ya
Muungano wetu kwa kuzingatia Serikali sasa imeshahamia Dodoma na tayari
Watendaji wake wapo huku hivyo tuitumie fursa hii kuwaalika Wananchi
wote kuudhuria kwa wingi ili kuifanikisha na kuonesha Umoja
wetu.”Alisistiza Waziri
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) January Makamba ametoa wito kwa Watanzania wote wajitokeze
kwa wingi kwenda kuangalia mafanikio yaliyotokana na uwepo wa Muungano
huo.
“Muungano
huu umetupa mafanikio mengi ikiwemo; kuijengea nchi heshima, kuwepo kwa
Katiba, kuimarika kwa Taasisi za kimuungano, ongezeko la masuala ya
kimuungano kutoka 11 hadi 22, ongezeko la usalama, Kuwepo Mfumo dhabiti
wa kushughulikia changamoto za Muungano na ongezeko la ushirikiano kwa
masuala yasiyo ya Kimuungano.”Alieleza waziri Makamba.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana alipongeza jitihada za
Ofisi ya Waziri Mkuu hususan Kitengo cha Maadhimisho kwa kushirikiana na
Ofisi yake kwa kuratibu na kuhakikisha maandalizi yote yamekalika kwa
wakati uliopangwa.
“Niipongeze
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada zake kuiratibu siku hii muhimu kwa
Taifa letu, na nitoe wito kwa Wakazi wa Dodoma na walioko nje ya Mji
kuonesha mfano kuja kwa wingi ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.”Alisisitiza Mhe.Rugimbana.
CHANGAMOTO
ZA MUUNGANO ZATATULIWA KWA KIASI KIKUBWA : MAKAMBA
Na;
Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa - Dodoma
Waziri wa Nchi
anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano
wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15
mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano unaotimiza miaka
53 wiki ijayo.
Waziri Makamba
amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa
habari ulioandaliwa na waratibu wa sherehe
za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na
kusimamiwa na Waziri Mwenye dhamana Mhe Jenista Mhagama.
Mhe. Makamba amezitaja
changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto
unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa
swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa
kwa taratibu za kisheria.
Alisema kuwa changamoto
nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya Pamoja ya fedha.
Awali akizungumzia
Muungano huo unaotimiza miaka 53, Waziri Makamba Alisema kuwa umekuwepo kisheria na umerasimisha
udugu na ushirikiano uliyokuwepo kati ya Bara na Visiwani.
Mkutano huo wa
waandishi wa habari uliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana
Ajira na Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan
Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama akizungumza na
waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili
2017.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan
Rugimbana.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na
watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama wakati akizungumza nao kuhusu maandalizi
ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari
leo Mjini Dodoma kuhusu matukio mbalimbali yatakayokuwepo katika Maadhimisho ya
Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika
Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na mwishoni ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana
akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maandalizi ya
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017 na kuwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,
Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO
Dkt.Hassan Abbas akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho
ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika
Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.KUlia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama ,Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera
na Uratibu) Dkt.Hamis Mwinyimvua(kushoto)
na Mkurugenzi Idara ya Uratibu na
Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi ya Waziri Bi.Flora Mazilengwe wakifurahia jambo
katika Mkutano na waandishi wa Habari kuhusu
juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Prof.Faustine Kamuzora akifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba wakati wa mkutano na waandishi
wa Habari kuhusu maandalizi ya
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017. Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO,
DODOMA.
Post a Comment