Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Manara amekutana na kitanzi cha TFF
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
KAMATI ya maadili imemfungia Afisa Habari wa timu ya Simba Haji Manara kutojihusisha na shughuli za Mpira ndani na nje ya nchi kwa muda ...
KAMATI ya maadili imemfungia Afisa Habari wa timu ya Simba Haji Manara kutojihusisha na shughuli za Mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) sawa na mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tisa (9) kutokana na kukutwa na hatia kwenye makosa yote matatu aliyokuwa akikabiliwa nayo.
TFF ilimfungulia mashtaka ya kinidhamu yenye makosa matatu kwenye kamati ya maadili. Kosa la kwanza ni kuongea maneno ya kashfa kwa viongozi wa TFF, kosa la pili kuchochea ukabila na kosa la tatu ni kukosoa maamuzi ya TFF kupeleka suala la Mohammed Fakhi kwenye kamati ya Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Jerome Msemwa akitangaza hukumu hiyo alisema katika shitaka la kwanza Manara amefungiwa mwaka mmoja na faini milioni moja wakati lile la pili amefungiwa miezi mitatu faini milioni tatu na la tatu amepigwa faini ya milioni tano au kutojihusisha na soka kwa miaka saba.
Jerome alisema mshitakiwa alipewa hati ya mashitaka na kutakiwa kuhudhuria kwenye kikao hicho lakini alishindwa kutokea bila kuwa na sababu za msingi. Ila Manara yuko huru kukata rufaa kama hajaridhishwa na hukumu hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top