Mastaa wa muziki pamoja na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi
hapo jana, katika mazishi ya baba wa staa wa muziki, Belle 9 aliyefariki
akiwa hospitalini mkoani humo usiku wa Machi 18 akipatiwa matibabu
baada ya kugongwa na pikipiki.
Belle akiwa na wasanii pamoja na wadau mbalimbali mbele ya kaburi la marehemu baba yake baada ya mazishi.
Meneja wake, Jahz Zamba, aliiambia Bongo5 kuwa, Mzee Damian amefariki
dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko
mjini Morogoro alikokuwa akiishi.
Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa
hospitali. Dereva wa boda boda naye aliumia vibaya ikiwemo kuvunjika
taya na kujeruhiwa kichwa.
Jahz alisema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa
kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini
zilikosekana kwenye hospitali hiyo.
Ni pengo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake, kwakuwa mara nyingi
amekua akidai baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Muimbaji
huyo anayetokea Morogoro alimtaja mzazi wake huyo kuwa ni mtu
anayemuinspire kwa mambo mengi.
Tunampa pole Belle kwa msiba huu mzito na Mungu ailaze roho ya baba yake mahala pema peponi.
Stamina, Afande Selle na wadau wengine.
Mtayarishaji wa muziki, Mona (kushoto) akiwa Morogoro.
Mamia wamzika Baba yake Belle 9
Title: Mamia wamzika Baba yake Belle 9
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Mastaa wa muziki pamoja na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi hapo jana, katika mazishi ya baba wa staa wa muziki, Belle 9 aliyefariki...
Post a Comment