Wananchi
Wilayani Handeni wametakiwa kutilia mkazo suala la kuwapeleka watoto
kupata chanjo mara zinapotangazwa ili kuendana na msemo wa kinga ni bora
kuliko tiba.
Rai
hiyo ilitolewa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo ya polio wenye
kauli mbiu ya “jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya” uliofanyika
katika Zahanati ya Mumbwi iliyopo Katika Kijiji cha Mumbwi kata ya
Komkonga.
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe mbaye pia alikuwa mgeni rasmi
alieleza kuwa Serikali inajitahidi kutoa chanjo bure hivyo wananchi pia
wanao wajibu wa kuhakikisha wanapeleka watoto wao kupata chanjo hizo
kwaajili ya ustawi wa afya za watoto.
“Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni inazo chanjo za kutosha, chanjo mkoba na chanjo
tembezi zitafika kwenye maeneo ambayo bado hayana zahanati ili
kuhakikisha watoto wote Wilayani Handeni wanachanjwa” alisema Mh.
Gondwe.
Aidha
, aliwataka Maafisa Tarafa, Watendaji Kata na Vijiji kuweka agenda ya
usafi na mazingira, afya na bima kuwa ndelevu katika viko vyao vya
Vijiji.Akizungumzia suala la malaria kwenye siku ya maadhimisho ya siku
ya malaria duniani Mh. Gondwe alisema kila mwanachi anawajibu wa kutunza
mazingira na kutokomeza mazalia ya mbu ili kutokomeza kabisa ugonjwa
huo.
“Chanjo
zinatolewa bure,vipimo vya malaria vinatolewa bure na baadhi ya dawa za
malaria bure lakini ni vyema kila mwananchi kuwa na bima ya afya ili
kuepuka gharama za matibabu na kuhakikisha kuwa suala la afya haliwi
tatizo kwenye Wilaya ya Handeni”alisema Mh.Gondwe.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Simon Mdaki alieleza kuwa
chanjo zingharamiwa hivyo ni vyema wananchi kutambua umuhimu wa kupeleka
watoto kupata chanjo.mtoto akiuguwa wasikimbilie kuhisi motto kalogwa
badala yake wamuwahishe hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa
unaomsumbua. Polio sio ugonjwa wa kulogwa ni chanjo ndio inapaswa
kupatiwa motto angaliakiwa mdogo.
Aidha
aliwataka wananchi wote kuzingatia kinga na kutunza mazingira
kutokomeza madimbwi na mazalia ya mbu huku wakizingatia matumizi bora ya
vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni ilikuwa na lengo la kutoa chanjo kwa watoto 2883
badala yake wamechanja watoto 3435 sawa na asilimia 119 (kwa kipimo cha
penta) mbali na changamoto mbalimbali zinazokabili Idara ya Afya.
Uzinduzi
huo ulipambwa na kikundi cha ngoma za asili cha chanika kofi na
kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya wakiwemo
Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Chama CCM, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya Handeni, Wataalamu wa Afya na watendaji wa
Halmashauri.
Alda Sadango.
Afisa Habari.
Halmashauri ya Wilaya Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizindua zoezi la utoaji chanjo Kwa watoto kwa kumpatia mtoto matone ya chanjo ya polio.

Mh Godwin Gondwe akiwa kwenye picha ya pamoja na walezi wahakikishe watoto aliowapatia chanjo huku akiwa amembeba mtoto ikramu mbarouk Mara baada ya kutoa chanjo Kwa watoto wao.

Viongozi mbalalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakiongozwa na mkuu wa Wilaya Mh Godwin Gondwe wakiwa wamebeba watoto waliopatiwa chanjo

Baadhi ya wazazi waliojitokeza kuleta watoto wao kupatiwa chanjo.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wakati kijiji cha Kitumbi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw Ramadhani Diliwa akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo.

Kaimu Mkurugenzi Bw Simon Mdaki akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitumbi
Post a Comment