Simbu, ambaye alishika nafasi ya 5 katika mashindano hayo makubwa Duniani, amewataka wakimbiza upepo wengine wenye ndoto kama zake ni lazima wafanye mazoezi kwa juhudi kabla ya kushiriki mashindano yoyote makubwa. Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kumpongeza huko Mkoani Arusha.
Hata hivyo nyota huyo anayeiwakilisha vyema taifa, katika mchezo wa riadha siku za hivi karibuni amewataka wadau wajitokeze kushirikiana na serikali kuwekeza zaidi katika mchezo huo, kwani yeye ni jibu tosha la zao lililopatikana katika uwekezaji wa muda mfupi.
Felix Simbu ametumia saa 2, dakika 9 na sekunde 9 na kushika nafasi hiyo ya tano.
Ambapo inaonyesha mwanariadha anayeshika nafasi ya tano katika mashindano hayo anaibuka na kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).
Post a Comment