WAZIRI NAPE MGENI RASIMI FAINALI ZA ULEGA CUP ZITAKAZOFANYIKA MACHI 5 MKURANGA
Timu
ya kata ya Tengelea, Tengelea FC imefunzu kuingia katika fainali ya
Ulega Cap baada ya kuifunga Timu ya Mwandege FC bao 1 – 0 katika
mcheezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana .
Bao
la timu ya Tengelea lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia
mchezaji wao Andew Joseph aliyepokea cross ambayo ndio ilipa ushindi
timu hiyo.
Timu
ya kata ya Tengelea, itaingia fainali kwa kukipiga na timu ya Kisiju na
mechi itanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Mwandege FC na
Lukanga FC.
Mgeni rasmi katika fainali za Ulega CUP ni Waziri Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye.
Akizungumza
na waandishi wa habari muandaji wa mashindano hayo Mbunge wa Mkuranga,
Abdallah Ulega amesema kuwa mashindano yameibua vipaji ya vipya.
Amesema kuwa inahitaji uwekezaji katika michezo kutokana na vijana kuonyesha vipaji vyao ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji
wa timu ya Tengelea iliyopata ushindi wa kuingia fainali ya Ulega CUP
katika mchezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana.
Mbunge
wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji
wa timu ya Mwandege ambao ni washindi wa tatu katika mashindano ya Ulega
Cup baada ya kupata kichapo jana na timu ya Tengelea katika mchezo
uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Vijana wakionyesha vipaji vyao katika mashindano ya Ulega CUP katika
mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Mashabiki
wakiwa juu ya miti wakifatilia mpira kati ya timu ya Tengelea na
Mwandege FC katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi
Mkuranga.
Post a Comment