TNRF yazindua mpango mkakati wa Ardhi
Kamishna
wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary
Makondo(aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mpango
mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania ambao utajumuisha mradi wa
majaribio katika mikoa mbalimbali kuona kama utawezekana maana swala la
upatikanaji wa ardhi imekuwa ni changamoto kubwa sana hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Joseph Olila akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania
uliodhaminiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania ili kuweza kupatikana kwa
ardhi hasa maeneo ya vijijini .
Mkurugenzi
Mtendani wa Taasisi ya MVUWATA ya Morogoro, Steven Ruvuga akizungumza
jinsi wanavyoweza kuhamasisha watu kwenye matumizi mazuri yaardhi pamoja
na kutatua migogoro ya ardhi kwenye mkutano uliofanyika kwneye ukumbi
wa Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam.
Bwana Alain Essimi Biloa akitoa mada juu ya matumizi mazuri ya ardhi kwenye jamii hasa kwa wananchi waishio vijijini
Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye kongamano lililofanyika leo katika Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo
Baadhi
ya wadau wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi
unaoratibiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF).
Meneja
Program wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Zakaria Faustine
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania ambao utajumuisha mradi wa majaribio katika mikoa mbalimbali
Afisa
Program za Ardhi Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF),Godfrey Massay
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati waliojiwekea kama
Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Kamishna
wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary
Makondo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kufanya uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi utakaoleta tija kwa wananchi hasa vijijini.
Picha ya Pamoja
Post a Comment