Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Jumatatu hii amekabidhiwa na kuzindua barabara ya kilometa 1 iliyojengwa kwa kiwango cha zege ambayo inaonganisha kati ya Kurasini na barabara ya Kilwa Road.
Akiongea katika makabidhiano hayo Operation Manager wa kampuni hiyo, Bw. Maswingo alisema anayofuraha kumkabidhi mkuu wa mkoa barabara hiyo ya kimometa 1 ambayo inaonganisha katika ya Kurasini na Kilwa Road ikiwa imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na aina ya magari ambayo yanatumia barabara hiyo.
“Hii barabara aliizindua mkuu wa mkoa mwaka jana mwezi 12 na sasa hivi tunamkabidhi ikiwa imekamilika. Barabara hii ni kiungo muhimu katika eneo hili bila shaka itachangia kuchochote maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa ni barabara hii ni kiungo muhimu,” alisema Mwaswingo.
Kwa pande wa mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alisema barabara hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa itawarahishia wafanyabiashara kutoa mizigo yao bandarini kwa urahisi.
“Ni barabara muhimu sana lakini ilikuwa ni barabara mbovu na isiyopitika hasa katika mazingira ya nyakati za mvua kama hizi. Kwahiyo niliwatafuta hawa ndugu nikawaomba namna mbavyo wanaweza kutoa mchango wao katika kuhakikisha hii barabara inapitaka vizuri na walinikubalia chini ya mkurugenzi wa na kampuni yao kwamba watatoa mchango wa kuiboresha Dar es salaam mpya kwa namna mbavyo wanaona wao inafaa,” alisema RC Makonda.
RC Makonda akikagua barabara hiyo
Pia RC Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango huku akidai kampuni zitakazotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka mitatu.
“Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi 6 haijapita”.
Post a Comment