Kikwete ateua watu tisa kusimamia bodi ya Taasisi yake
Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete amechagua na kuwataja wajumbe tisa wa Bodi ya wadhamini wa Taasisi ya Mfuko wa maendeleo ya Jakaya Kikwete (JMKF).
Aliwachagua wajumbe hao wakati akizindua bodi ya wadhamini wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Amewataja wajumbe wa bodi hiyo kuwa ni pamoja na Balozi Ombeni Sefue, Profesa Rwekaza Mukandala ambaye ni makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine ni Balozi Mwanaidi Sinare Majaar, Profesa William Mahalu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Utabibu, Bugando Mwanza.
Wajumbe wengine ni Abubakar Bakhresa, Genevieve Sangudi, Dato’ Sri Idris Jala waziri asiyekuwa na wizara maalumu ofisi ya waziri mkuu wa Malaysia, Balozi Charles Stith, balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, pamoja na Dk Carlos Lopez ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (UNITAR).
By: Emmy Mwaipopo
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment