MKUTANO MKUU WA NNE WA MWAKA WA MAGEREZA SACCOS WAFANYIKA BWALO KUU LA MAAFISA MAGEREZA, UKONGA - DAR ESALAAM
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha
Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza(TPS SACCOS LTD) akitoa maelezo
mafupi kabla ya kumkaribisha Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika afungue rasmi Mkutano
Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd leo Machi 13, 2016 uliofanyika kwa siku moja katika
Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila ambaye ni Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Lindi akitoa hoja ya kuthibitisha Notisi ya Mkutano Mkuu mbele ya
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nne uliofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa Bwalo Kuu
la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Bw. Colin Nyakunga akitoa salaam ya Ushirika
kabla ya kutoa Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd leo
Machi 13, 2016 uliofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza
Ukonga – Dar es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la
Magereza wenye vyeo mbalimbali ambao ni Wanachama wa TPS SACCOS LTD kutoka Mikoa
yote Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi katika Mkutano huo.
Meza Kuu wakiwa wameketi wakifuatilia zoezi la Utambulisho wa Wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa nne wa TPS SACCOS Ltd leo Machi 13, 2016 uliofanyika kwa siku moja
katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam (katikati) ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(Kulia) ni Kaimu Mrajis wa Vyama
vya Ushirika, Bw. Colin Nyakunga(kushoto) ni Mwenyekiti wa TPS SACOSS LTD, SACP.
Gideon Nkana.
Sekretarieti ya Mkutano Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd wakiwajibika kama
inavyoonekana katika picha.
Mwenyekiti TPS SACCOS Ltd, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon
Nkana akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(Kulia).
Baadhi ya Watendaji wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la
Magereza wakiwajibika katika Mkutano huo kama inavyoonekana katika picha.
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Bw. Colin Nyakunga(wa nne toka kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd
uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam(wa
nne toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu kulia)
ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa pili kulia) ni Naibu
Kamishna wa Magereza, Edith Mallya(wa pili kushoto) ni Mwenyekiti TPS SACCOS Ltd,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana(Picha zote na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza).
Post a Comment