Kesi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums yarushwa hadi Machi 9
Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao maarufu, Jamii Forums, Maxence Melo imeahirishwa mpaka Machi 9 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao huo, kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hakimu Mkazi Victoria Nongwa anayesimamia kesi hiyo kutokuwepo.
Mkurugenzi huyo anakabiliwa na shitaka la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa, kitu ambacho ni kinyume na sheria, shitaka lingine ni kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao pamoja na kusajili tovuti ya Jamii Forums kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo pia serikali inadai ni kinyume cha sheria.
Post a Comment