Alhamisi hii Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga, Yusuph Manji alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku akisomewa shitaka moja la kutumia dawa za kulevya.
Manji akiwasili kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Hata hivyo Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 na kudhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena March 16 mwaka huu.
Tazama video na picha zaidi hapa chini picha za Manji wakati akiwa mahakamani mahakamani pamoja na zile za mashabiki wa Yanga.
Manji akitolewa mahakamani baada ya kupata dhamana
Viongozi wa Yanga na mashabiki wakisubiri kusikiliza kesi ya Manji
Wanasheria wa Manji, kushoto ni Msemwa na kulia ni Alex Mgongolwa
Wanasheria wa serikali wakiingia mahakamani
Manji akiingia kwenye ofisi ya Hakimu Mkazi kwa ajili ya kusauni fomu za dhamana
Mashabiki wa Yanga wakiongozwa na Mama Yanga wakijaribu kulizuia gari la Manji ili ashuke wakati akitoka mahakamani baada ya kupata dhamana
Mashabiki wa Yanga wakisoma dua baada ya Manji kupata dhamana
Post a Comment