Wanyama atajwa mwanasoka bora Afrika mwezi wa January
Mkenya anayeichezea timu ya Tottenham Hotspurs, Victor Mugubi Wanyama ametajwa kama mchezaji bora wa Afrika(EPL player of the month).
Nahodha huyo wa Harambee Stars, aliweza kuwamwaga Yaya Toure,Victor Moses na Sadio Mane kwenye kinyang’anyiro hicho. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 25, ni muhimu sana kwa timu yake na amekuwa akionesha kiwango cha juu cha mchezo hivi karibuni.
Akiendelea hivi atakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika. Mwezi December, mchezaji wa Ivory Coast, Yaya Toure anayeichezea Manchester City alishinda tuzo hiyo.
Post a Comment