usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Shamra
shamra za Maadhimisho ya kusherehekea kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi
matukufu ya Zanzibar ya kwaka 1964 yaliyowakomboa Wakwezi na Wakulima
kutokana na madhila ya Wakoloni yameanza rasmi hapa Nchini kwa shughuli
za usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na
Pemba.
Usafi
huo uuliowajumuisha wananchi wa rika zote wakiongozwa na Viongozi wao
wa Wadi, Majimbo, Wilaya pamoja na Mikoa umefanyika mapema asubuhi kwa
kuweka mazingira safi katika baadhi ya sehemu zikiwemo Bara bara Kuu.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar
alijumuika pamoja na Wananchi hao katika usafi huo hapo Mtoni Kidatu
Wilaya ya Magharibi “A”.
Eneo
hilo limechaguliwa maalum na Uongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kufanya
usafi wa mazingira kutokana na Historia yake ya kuwa chimbuko Kuu la
kuibika kwa mripuko wa maradhi ya kuharisha na kuambukiza ya Kipindu
pindu.
Akizungumza
na Viongozi pamoja na Wananchi walioshiriki kwenye zoezi hilo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema usafi wa
mazingira ni suala la msingi linalopaswa kuendelezwa miongoni mwa
Wananchi wenyewe katika mazingira yao ya kila siku.
Balozi
Seif aliendelea kusisitiza kila mara anaposhiriki kwenye masula ya
usafi wa mazingira kwamba bado utaratibu wa kufikiria kufanya usafi
siku moja ya kila Mwezi una manitiki yake katika dhana nzima ya kuweka
mazingira safi yanayochangia uwepo wa uhakika afya za Wananchi Mitaani.
Alisema
yapo Mataifa mengi Duniani yaliyofanikiwa kujiwekea utaratibu mzuri wa
kutekeleza mpango wa usafi wa mazingira yakiwemo pia yale ya Bara la
Afrika akiitolea mfano Rwanda ambayo Wananchi wanastahiki kuuiga mfano
huo muhimu kwa faida ya Taifa.
Akigusia
uvamizi holela wa maeneo mbali mbali ya ardhi nay ale ya wazi hapa
Nchini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema tabia hiyo mbaya
inaathiri utaratibu mzuriunaowekwa na Serikali katika suala la Mipango
Miji.
Balozi
Seif alitahadharisha kwamba ujenzi holela unafanywa na baadhi ya watu
kwa tamaa zisizo na msingi kwa Taifa na Wananchi wake hazitovumiliwa na
Serikali kupitia Taasisi zake kama Baraza la Manispaa pamoja na
Hamlashauri za Wilaya.
Aliupongeza
Uongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa hatua kubwa unaoendelea
kuchukuwa katika kuimarisha Mipango Miji itakayosaidia kurejesha haiba
ya Mji wa Zanzibar katika Nyanja ya Kihistoria.
Alisema
juhudi hizo ni vyema zikaungwa mkono kwa dhati na Wananchi kwa kutoa
taarifa pale wanapogundua uvunjaji wa sheria na taratibu zilizowekwa na
Serikali pamoja nja Halmashauri zake kwenye Wilaya zote za Unguja na
Pemba.
Mapema
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema
Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa na Halmashauri
zake zimetenga maeneo Matatu ndani ya Mkoa huo kwa ajili ya usafi wa
mazingira ndani ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 53.
Mh.
Ayoub aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Bara bara na Mkapa, Bara
bara ya Amani hadi Biziredi , Jang’ombe pamoja na Amani hadi
Mwanakwerekwe ambayo alisema hayamo katika utaratibu wa kufanyiwa usafi
wa mazingira.
Aliipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kugawa Mabaraza ya
Mji kitendo ambacho kimeonyesha mwanzo mzuri wa kubadilika hali ya
mazingira na usafi wa Halmashauri mpya zilizoundwa.
Akigusia
eneo la Mtoni Kidatu liloteuliwa maalum kwa ajili ya usafi wa mazingira
katika maadhimisho ya kuanza kwa sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
kutimia Miaka 53, Mh. Ayoub lengo ni kuwashajiisha wananchi wa eneo
hilo kupenda kufanya usafi wa mazingira kila mara.
Alisema
Mtoni Kidatu na Mto Pepo ni maeneo hatarishi ya kuwa chanzo kikuu cha
mripuko wa maradhi ya kuambukiza ya Kipindu pindu yanayosababishwa na
mazingira mabovu ya uchafu.
Maadhimisho
ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia miaka 53
yanatarajiwa kufikia kilele chake Tarehe 12 Januari 2017 katika Uwanja
wa michezo wa Amani Mjini Zanzibar.
Post a Comment