“Paul Pogba atakua kama Memphis Depay”
Ni ngumu sana kuweza ku-balance maisha ya u-star kama hollywood na kuwa mwanamichezo mkamilifu unayeleta matokeo. Legend wa Holland Ruud Gullit amemuonya Pogba kwamba yupo njiani kuwa kama Depay kwenye siku zijazo.
Ruud Gullit anasema kwamba Pogba anafanya makosa ku-focus kwenye mambo ya fashion na kuacha ku-focus kwenye soka ambayo ndio kazi yake kubwa. Tumemuona mchezaji anayeendesha Rolls Royce muda wote akiondoka Manchester united baada ya kushindwa kuonyesha uwezo.
Pogba amekua akitengeneza vichwa vya habari kwa kuzindua mavazi yake akishirikiana na Adiddas na kuwa mchezaji wa kwanza Premier league kutoa Emoji zake.
Gillit alisema,“Pogba anaenda kwenye njia moja ambayo Memphis amepitia. Anaweza kuwa mchezaji wa gharama zaidi duniani lakini hiyo haijalishi kama unatumia muda wako mwingi kupata rangi nywere zako zaidi ya kazi yako uwanjani”
“Memphis alikuwa anakosolewa sana kwasababu aliona ni vizuri sana kuweka muonekano wake kwa njia mbalimbali zaidi ya soka lake. Anatakiwa kujua vitu vya uwanjani vinaanza kabla ya kitu kingine chochote. Ushauri wangu ni kwamba soka lianze kabla ya kutaka umaarufu kwenye vitu vingine”.
Gillit alisema pia magoli ya Ibrahimovic yamemsaidia Jose kuepuka aibu kama ya Van Gaal zaidi ya magoli ya Pogba.
Post a Comment