Barnaba: Nimeifumua upya album niliyopanga kuitoa ili kuipa nguvu zaidi
Barnaba amedai kuwa amelazimika kuifumua upya album yake aliyokuwa amepanga kuitoa mwaka jana ili kuipa nguvu zaidi.Mwaka jana, muimbaji huyo aliahidi kuitoa album yake aliyokuwa ameipa jina ‘Nane Nane’ kwenye siku wa Wakulima (August 8) lakini aliahirisha baada ya sponsor aliyekuwa ameingia ubia kwenye album hiyo kubadilisha mawazo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Loudspika cha Africa Swahili FM, Morogoro, Barbaba amedai kuwa ushindani toka kwa wasanii wapya ni sababu za kujipanga upya.
Barnaba amedai kuwa siku ya Valentine’s atatoa bonus track ambayo huenda ikabeba jina la album hiyo. Juu ni interview nzima aliyofanya na mtangazaji Ergon Elly.
Post a Comment