Alichokisema Micho baada ya Uganda kutupwa nje AFCON 2017
Kocha wa
Uganda Milutin Sredojevic ‘Micho’ amekiri ni ngumu kuamini kuwa timu
yake imetupwa nje ya michuano ya mataifa ya Afrika.
Hatua hii ya mashindano inahitaji umakini wa hali ya juu hususan
kwenye michezo ambayo inaamua nani asonge mbele na nani anabaki,”
anasema Micho baada ya kikosi chake kuondoshwa kwenye michuano kwa
kipigo cha goli 1-0 na Misri.“Tumekuja kwenye mashindano haya baada ya miaka 39 na tumejifunza kitu japo ni ngumu”.
“Ukipoteza huku umecheza vizuri unakubali, lakini kwa hali hii ni ngumu sana kukubali.”
Matokeo ya kufungwa mara mbili mfululizo kwenye kundi lao, yanawaacha Uganda chini kwenye msimamo wa Kundi lao huku wakiwa hawana matumaini tena ya kusonga mbele baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali hizo tangu mwaka 1978
“Tulishindwa kuwa makini hadi dakika ya mwisho tukaruhusu counter-attack na kwa uzoefu na ubora wa Mohamed Salah akaonesha tofauti,” anasema Micho.
“Tulikuja hapa kucheza mechi tatu za michuano hii, mechi ya kwanza tukapoteza kwa mkwaju wa penati dhidi ya Ghana na mechi ya pili tukapoteza dakika ya mwisho kwa shambulizi la kushtukiza.”
Jumatano hii, Uganda sasa itacheza mchezo wa mwisho kukamilisha ratiba dhidi ya Mali.
“Sasa tunatakiwa kuangalia makosa yetu na kusonga mbele kuona namna gani tutacheza mechi yetu ya mwisho. Ni vigumu kusema nani na nani watacheza mchezo wa mwisho, tuna majeruhi (golikipa Denis Onyango),” anasema Micho.
“Tutaona namna ya kucheza mechi yetu ya mwisho lakini malengo yetu yanabaki palepale kwamba tunataka kurudi nyumbani kwa heshima tukiwa na ushindi.”
Post a Comment