Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Aubameyang ameshindwa kuibeba Gabon
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Aubameyang ameshindwa kuibeba Gabon Gabon imekuwa mwenyeji wa nne kutolewa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwenye hatu...

Aubameyang ameshindwa kuibeba Gabon

Aubameyang
Gabon imekuwa mwenyeji wa nne kutolewa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwenye hatua ya makundi baada ya kutoka suluhu na Cameroon kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A na kuwaacha Cameroon wakisonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Pierre-Emerick Aubameyang alipoteza nafasi ya wazi kuifungia Gabon bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza akiwa yeye na goli.
Gabon waliingia kwenye mechi hiyo wakijua ushindi pekee ndio utawahakikishia nafasi ya kusonga mbele kutoka Kundi A lakini wamejikuta wakiyaaga mashindano baada ya kupata sare tatu mfululizo.
Burkina Faso ni timu nyingine iliyofuzu kucheza robo fainali kutoka Kundi A baada ya kuifunga 2-0 Guinea-Bissau matokeo ambayo yamewaweka kileleni mwa kundi juu ya Cameroon kwa tofauti ya magoli.
Aubameyang ambaye ni star wa Borussia Dortmund, ameongezewa machungu hasa akikumbuka michuano ya mwaka 2012 ambapo alikosa mkwaju wa penati ili kuisaidia timu yake kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top