Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Claudio Ranieri: Natamani kuona Conte akishinda taji la EPL
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Claudio Ranieri: Natamani kuona Conte akishinda taji la EPL Kocha wa klabu ya Leicester City, Claudio Ranieri amesema anatamani kuona ra...

Claudio Ranieri: Natamani kuona Conte akishinda taji la EPL


Kocha wa klabu ya Leicester City, Claudio Ranieri amesema anatamani kuona raia mwenzake wa Italia Antonio Conte ambaye anaifundisha Chelsea ashinde taji la ligi ya Uingereza.

“Kama mkufunzi wa zamani wa Chelsea na shabiki wa Italia, natumai Conte atatimiza lengo hilo. Ameonesha kwamba makocha wa Italia ni stadi sana. Ranieri ana mkataba Leicester hadi 2020 lakini anakubali kwamba nafasi yake katika klabu hiyo haiko salama, licha ya kufikia ufanisi wa kushangaza msimu uliopita,” amesema Ranieri.
“Natumai nitasalia England. Ninahisi vyema hapa, ingawa katika kandanda mnakuwa juu kwenye nyota leo na kesho yake mnajipata chini sakafuni. Kwa hiyo usiwahi kudhania umefika,” ameongeza.
Ranieri, 65, aliongoza Leicester kushinda taji hilo msimu uliopita kwa njia ya kushangaza. Lakini kwa sasa Leicester ipo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa nyuma ya pointi 34 na vinara wa ligi hiyo Chelsea

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top