Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: THOMAS MASHALE ADAIWA KUUWAWA DAR ES SALAAM.
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika),amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko mae...

thomas-mashali

Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika),amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony  Lutta,ameiambia ‘Fullshangweblog’ kuwa taarifa walizozipata ingawa bado  hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.

Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo  mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo  ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili.

Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.

Mashali ambaye  jina lake la  kuzaliwa ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.

Marehemu ameacha mke na watoto.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top