Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: JACKSON MAYANJA HATUNA WASIWASI NA STAND UNITED JUMATANO HII MCHEZO WA LIGI KUU TANZANIA BARA.
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya kuvunja mwiko kwa kuifunga timu ya Mwadui FC kocha nsaidizi wa Simba Jackson Mayanja ametamba kuwa Stand lazima wakae siku ya Ju...
Baada ya kuvunja mwiko kwa kuifunga timu ya Mwadui FC kocha nsaidizi wa Simba Jackson Mayanja ametamba kuwa Stand lazima wakae siku ya Jumatatu mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara utakaochezwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mazoezi Leo Mayanja amesema kuwa wana wajua wapinzani wao kubwa ni timu tishio hasa wakiwa katika uwanja wao wa CCM Kambarage kwani msimu huu wameweza kuzifunga timu kubwa kama vile Yanga na Azam FC hivyo tunauchukulia mchezo huu kama Fainali kwetu.
“Unajua msimu huu kila timu imejinga vizuri ila sisi tupo imara zaidi ya timu nyingine na lazima tupate matokeo ya alama tatu muhimu kwani ndio kauli yetu na wachezaji wanajua nini wanatakiwa wakifanye bila kuwabeza wapinzani wako vizuri na tunapambana katika viwanja vya mikoani kwani ni vibovu ila hilo halitupi shida sisi’alisema Mayanja
Stand wamekuwa wagumu kufungika wakiwa katika uwanja wa Kambarage na mpaka kupewa jina la kutumbua vigogo na tayari tambo zimeanza kutamba kila upande na wapiga debe hao hawajapoteza mchezo wowote wakiwa nyumbani hivyo ni mchezo utakaotazaamwa na watu wengi zaidi siku ya Jumatano.
Simba wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika uwanja huu huo na mpaka sasa ndio timu pekee kwenye Ligi iliyofungwa mabao machache matatu na kutokupoteza hata mchezo mmoja ipo kileleni ikiwa na alama 32.
ruvushooting-simba

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top