Baada ya kuwapigilia msumari wa moto Mbao Fc,timu ya Yanga
imetuma salamu katika mkoa wa Mbeya kwani inatarajia kucheza michezo
miwili wiki hii ikianza na Mbeya City Jumatano na Jumamosi kucheza na
Tanzania Prisons katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza Kaimu katibu wa klabu hiyo Baraka
Deusdedit,amesema kuwa maandalizi yote ya kuelekea Mbeya yamekamilika na
timu inaweza kusafiri wakati wowote huku ikiwa na morali ya kwenda
kuchukua alama sita mbele ya wenyeji kwani tuna kikosi kipana zaidi ya
wenyeji.“Dhamira yetu ni kuchukua alama zote sita na pia tuna rekodi nzuri kwa timu zote mbili hatuwezi kuzibeza hivyo tumejipanga kupambana kwa kila hali na mwisho tuweze kuibuka na ushindi na pia tunajua mazingira ya ugenini kutokana ubovu wa viwanja na kwa kuona hivyo benchi la ufundi linajua litumie mbinu gani ikiwa ni ubovu wa miundombinu’alisema Deusdedit
Taarifa za ndani kuwa Yanga huenda ikasafiri kesho kwa njia ya shirika la Ndege tayari kabisa kwa mapambano ya mechi zote mbili huku ikiwa na rekodi nzuri mbele ya Mbeya City kwani hawajawahi kufungwa na timu hiyo tangu ipande Ligi ingawa imekuwa ikikumbana na wakati mgumu kwa Tanzania Prisons hivyo mchezo huu utakuwa mkali na upinzani na Mbeya City wakita kuandika rekodi kwa mabingwa hao.
Yanga anaenda kucheza mkoani
Mbeya huku akiwa na alama 27 katika msimamo wa Ligi kwa mechi 12
alizocheza wakati wenyeji wote wana alama 16 wakiwa na tofauti ya mabao
ya kufunga na kufungwa kwani Prisons wapo nafasi ya 7 na Mbeya City
nafasi ya tisa ngoja tuone Yanga ataweza kuondoka na alama 6.

Post a Comment