WANAKIKUNDI
cha upakasaji mikoba, makawa, vipochi vya ukili na upandaji miti cha
‘Subira njema’ kilichopo kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani Pemba,
ambao wengi wao ni watu wenye ulemavu, wakiwa kazini katika kazi yao
hiyo ambapo mkoba mmoja wa kisasa wenye zipu ni shilingi 20,000 hadi
shilingi 25,000, (picha na Haji Nassor, Pemba)
WAJASIRIAMALI
kisiwani Pemba, wakiwa na sabuni za michi, nje ya ukumbi wa kiwanda cha
mafuta ya Makonyo Wawi Chakechake baada ya kuhitimu mafunzo hayo,
(Picha na Haji Nassor, Pemba)
NA HAJI NASSOR, PEMBA
“………kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda…………..”
Huu ni msemo maarufu ambao unatumika katika visiwa vya Unguja na Pemba na hata kuleTanzania bara kwa baadhi ya maeneo.
Hapo
zamani za kale, wazee wetu walikuwa wanapenda zaidi kutumia misemo
kuliko bakora, kwa lengo la kuwafundisha na kuwaasa wanaowalea
‘’Maskini enzi zetu zimeshapita ‘’baadhi ya wazee wenye umri wamekuwa wakisema kwa karne hii.
Katika
zama hizi za Sayansi na Teknologia, si wengi ambao wanajua maana ya
misemo kadhaa, bali wengi wanaisikia tu na kutokua na jawabu rasmi.
Kwa hapo zamani misemo ni miongoni mwa bakora inayoweza kutumika kupiga mtu na mwenye akili timamu.
Ilikuwa
kwa hapo karne hiyo, misemo, inaweza kujua kwamba muda gani mtu
anatakiwa afanye nini, au ache kufanya jambo fulani, na kuwepo kwa
matunda.
‘Ama
kweli lishalo vuusha sidau’’, ndio maana leo hii waliowengi hawathamini
na wala hawajali misemo mbali mbali ya wazazi wetu ambao ndio
waliotuzaa.
Nisiende
mbali naogopa nisije nikageuka muazima jamvi…….. kwa wale wanaofahamu
ni kwamba mara husau lengo alilokwendea kwa jirani.
Nami
hapa naogopa na naheshimu nisije nikalisahau lengo langu ndani ya waraka
huu wa makala ambayo kwa hakika imenivutia na ndio maana nikaamua
kuiandika.
Lengo
hasa ni kikundi cha ushirika cha wanawake tena wenye ulemavu kilichopo
kijiji cha Changaweni wilaya ya Mkoani ndani ya Kisiwa cha marashi ya
karafuu.
“Ile
kauli isemayo………. wanawake wanaweza hapa haikwenda kombo kwa wanawake
hawa ukizingatia wao ni wenye ulemavu”, ni kweli kabisa wanaweza.
Si
wengine bali ni wanaushirika wa” Subira njema” wanawake ambao ni
walemavu na hapa nilitaka kujua historia ya wanaushirika hawa.
Nilianza kuweka kalamu na shati langu sawa, wakati nikizungumza na Amina Abdalla Said, yeye ndie Mwenyekiti wa wanaushirika hao.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo, ushirika wao ambao wanajituma usiku na mchana
kwa lengo lakupata riziki zao za halali, unajishughulisha na kazi mbali
mbali.
‘’Sisi
hapa twapakasa mikoba ya ukili lakini hii ya kisasa, nikamuliza hata
mikoba ya ukili kuna ya kisasa kumbe? akajibu ndioo huku akicheka.
Ushirika huo wa wanawake wenye ulemavu ulianza mwaka 2009, ukiwa na wanachama 10 wakiwemo wanaume wawili.
Kwa sasa unajishughulisha zaidi na utengenezaji wa sabuni za kufulia, kuoshea vyombo na kuogea na vipochi vya ukili.
Mwenyekiti
akizungumza na mwandishi wa makala haya, hapo Changaweni Mkoani,
hakuacha kuniambia kuwa wanatengeneza sabuni, je wanayo mashine.
Suali
hili nilimtupia tena Mwenyekiti huyo na bila ya kusita, akasema kuwa
‘tunatumia mikono na ndoo na hatuvai hata ‘glavu’ yaani kukinga
ngozi’’,alisema.
Hili
linatokana na kutokuwa na vifaa vya kutengenezea sabuni na kukumba na
kemikali kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya ‘kastik’ ambayo huichanganya
na malighafi nyengine.
Salama
Mwadini Juma ambae ni mwanachama wa ushirika huo wa ‘’Subira njema‘’
anasema hili hasa la kukosa mashine, limekuwa likiwahatarishia usalama
wa afya zao.
Anaona
kuwa, licha uzalishaji huo kuwa ni muda mrefu, lakini hadi sasa
hawajapatiwa mashine na kuendelea kuzalisha sabuni kwa kutumia mikono.
Akizungumzia
suala la soko la bidhaa hiyo Mshika fedha wa ushirika Nassra Yussuf
Khalifan, bado halijanyanyuka vyema, na wamekuwa wakiuza kwa
kubahatisha.
‘’Kwa
sasa wateja wetu ni hawa wanaokuja hapa hapa na kujinunulia, lakini lile
soko kubwa halipo, lakini pia kwa sababu bidhaa haziko kwenye
kiwango’’,alisema.
Ushirika
huo kwa sasa hauna ‘pekingi’ ya biashara zao, jambo ambalo huwenda
ikawa ni sababu moja wapo ya kutokuwa na soko la hali ya juu.
Miongoni
mwa aina sabuni wanazotengeneza kwa kutumia malighafi za mchachai,
mkaratusi, na nyengine baada ya kupewa mafunzo kupitia Umoja wa watu
wenye Ulemavu Zanzibar UWZ.
Ushirika
huu, kwa muda wa miaka nane sasa wanaendelea kuweka maisha yao rehani,
kwa kuendelea kutumia mkono yao kutengeneza sabuni kw aukosefu wa
mashine.
Soko
la uhakika hasa la bidhaa ya sabubu ndani ya ushirika huu, bado ni
kizungumkuti, maana hulazimika kuzikopesha ili zisijewaharibikia
mikononi mwao.
Sabuni
zenye thamani ya shilingi 150,000 sawa na michi 50 ya sabuni ziko
mikononi mwa wateja wao, maana hawana soko la uhakika na vyenginevyo
wakiogoa kuzikopesha ndio hawafikii malengo.
Hivi
karibuni kwa kutumia mikono yao, walizalisha sabuni boksi tano na kila
moja, huingiza michi 25, ambapo boksi tano zenye michi 75 sawa na
shilingi 225,000 walibahatika kuziuza.
Mbali
na mambo hayo ya usafi na povu, lakini ushirika huu ulionzishwa mika
nane iliopita, unajishughulisha na utengenezaji wa mikoba ya kisasa na
vipochi vya ukili ,mikeka na makawa .
Kwenye ushirika huu wanauza mkoba mmoja kwa bei ya shilingi 10,000 hadi shilingi 15,000 kutokana na ukubwa wa mkoba huiska.
‘Lakini
pia ipo mikoba mengine hii ambayo sio ya kileo sana hii tunauza kati ya
shilingi 8,000 hadi shilingi 7,000 alisema huku akiwa na mkoba mkononi
Nassra Yussuf.
Kwa
kwenye ushirika huo, pia kwa vile wajishughulisha na upakasaji wa
makawa, huwezi kulipata kama huna shilingi shilingi 3,500 au shilingi
4,000.
Ukija
kwenye zulia la usumba ambapo ushirika huu unatengeneza na kuliuza kati
ya shilingi 7,000 kwa moja, wakati mkeka mmoja ni wenye ukubwa ni
shilling.40,000.
Ushirika
huo wa wanawake baada ya kuhangaika huku na kule, kwa sasa umeshaweka
mikono yake wazi kwenye benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuwa na
‘Account’ namba 041207000765.
Kwa
mujubu wa mshikafedha wa ‘Subira njema’ Nassra anabainisha pia kibakuli
chao hicho hakiko kitupa maana kina akiba ya zaidi ya shilingi laki tano
(500,000).
Toka kuanza ushirika huo hadi sasa, hawajawahi kupata msaada wowote kutoka Serekalini, ingawa wameshaomba mara kadhaa.
Jambo
hilo linawashangaaza sana maana walitakiwa kuanzisha vikundi vya aina
hiyo, lakini kwa sasa mambo ni magumu, kwao kutokana na kuwa
hawakumbukwi.
‘’Maisha
ni safari refu na safari ni hatua ‘’, na hatua lazima unyanyue mguu
lakini sisi mguu wetu umekwama na tunahitaji kukwamuliwa’’, alifafanua
Mshikafedha huyo.
Sikutosheka na hayo nilitaka kujua changamoto ambazo zimewakabili, ili kuweza kujua jinsi ya kuwasaidia kupitia ukurasua huu.
Salama
Mwadini Juma ambae ni mjumbe katika ushirika huo wa wanawake wenye
ulemavu hakunyamaza kimya, akasubiri kila kitu kusemewa alinyanyua mdomo
tena kwa sauti akiwa na tamaa kubwa ya kupata msaada.
Bi
Salama anasema kuna changamoto mbali mbali ambazo zimewakabili katika
ushirika wao, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi.
‘’Ofisi
hatuna, sabuni mapaka leo twafanyia mikono, soko madhubuti ambapo haya
yanatukwaza sana’’,alieleza huku akiwa na masikitiko.
Asya
Ali Hamadi, ambaye nae ni mjumbe katika ushirika wa ‘’Subira njema‘’
suala la kufanyia sabuni ndani ya nyumba ya mwanachama ni hatari hata
kiusalama wa watoto wao.
Aliomba
Serekali kupitia Wizara ya Uwezeshaji kuwaangalia kwa jicho la huruma,
kwani wakiwapatia msaada wataweza kujiendeleza zaidi.
Lakini
aliwageukia wanawake wenzake wale ambao hawajishughulishi na chochote,
wajitume na waondokane na dhana ya kuwa mwanamke siku zote ni mtu wa
kukaa ndani.
Akasema
hiyo ni dhana potofu, na anaetaka kujua juu ya hilo afike ‘Subira
njema’ Changaweni, kwani wanawake wanaweza hata kama hawakuwezeshwa.
Ndio
hapa pakuanzia kwa Wizara yetu ya uwezeshaji, kwani kwa muda mrefu
wanawake walionekana hawawezi ndio maana wakabakia majumbani na
kuhudumia watoto.
Asha
Hassan Makame, ambae hajajiingiza kwenye kikundi chochote cha ushirika,
anasema natamani sana ingawa, changamoto anayoiona ni kutengwa kwa
kukoseshwa vifaa.
“Vipo
vikundi vingi vya wanawake, lakini huona kama vile maisha yao
hayajabadilika yako sawa na yangu, sasa Napata wasiwasi wa kujiunga na
mimi’’,anasema.
Ingawa
Maulid Saleh Hamad wa Kiuyu yeye anasema kama yupo mwanamke Tanzania
hii hajajiunga na wala hanadhamira ya kujiingiza kwenye ushirika
amechelewa.
Mratibu wa TAMWA Zanzibar Mzuri Issa, yeye anaona ili uwanaharakati wa mwanamke utimie ni kukusanya nguvu zao pamoja.
“Baada
ya lazima sasa serikali ione umuhimu wa kuwasaidia vifaa kama hao
wanawake wenzetu wa Changaweni, ili wasonge mbele’’,alifafanua.
Mlekwa
Makame Hija wa Mkoani, anasema kama wanawake wakishajiunga pamoja na
kusaidiwa vifaa, wanaweza kupiga hatua moja kubwa ya kimaendeleo.
Ingawa
sheikh Nassor Khamis wa Mizingani anasema lazima wanawake waliopata
ruhusa kwa waume zao, kujiingiza kwenye vikundi hivyo, wasisahau wajibu
na majukumu yao, kama walivyo kwa wanaume.
Mkuu
Wa mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla anasema jambo la kwanza
ni mwanamke kukubali kujiingiza kwenye njia za kujikomboa.
“Unajua
serikali na hata wafadhili hupenda zaidi kuwasiaidia wanawake
waliojikusanya, sasa lazima tuhamasishahe kuefanya hivi, ili
tujikomboe’’,anashauri.
Naibu
Katibu mkuu wozara inayoshughulikia wanawake na watoto Mauwa Makame
Rajab ameutaka uongozi wa ushirika huo, wasisite kufika wizarani ili
kupata ufumbuzi.
“Waende
wizarani baada ya kujua gharama ya mashine ya kutengeneza sabuni, kisha
wanaweza kupewa maelekezo ya kuandika barua na kuomba
mkopo’’,anashauri.
Anesema
haipendezi na ni hatari kushika kemikali kwa mikono wakati wanajikomboa
kwa kutengeneza, sabuni waombe mkopo wanunue mashine.
Shemsa
Hakim Khamis ambae amejiari kwenye gari ya TAX eneo la uwanja wa ndege
Pemba, anasema lazima wanawake sasa wawe na njia ya kujikomboa.
“Maisha sasa yapaa, lazima kila mmoja ndani ya familia awe chanzo cha mapato, ili kuimarisha ndoa na familia’’,alishauri
Kwa
upande wake mjasiriamali anaejishughulisha na ususi wa mikoba ya kisasa,
wa Kiuyu wilaya ya Wete Nassra Salim Mohamed anasema hata kama mwanamke
ameolewa, lakini kujiingiza kwenye uwanaharakati ni lazima.
Asha Muhidin Mjaka wa Wawi ambae hajajiingiza kwenye ujasiriamali, anasema bado hajapata elimu ya juu ya jambo hilo.
“Mimi sijapa elimu na ndio maana hadi sasa naendelea na kilimo cha migomba, mihogo na mpunga peke yangu’’,alisema.
Mwakilishi
wa jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar UWZ Pemba Salum Abdallah,
amekitaka kikundi hicho cha ususi wa mikoba kuwashirikisha ili
kuwatafutia mashine.
“UWZ
ipo kwa ajili ya kuwahudumia wanachama wake, sasa wanapokwama waje ili
tuone wanaendeleza njia yao ya kujikomboa’’,alishauri.
Daktari
Makame Hassan Makame, anasema kemikali na mchanganyiko wa dawa nyengine
zikiingia kwenye ngozi ya mwanadamu husababisha madhara kadhaa.
“Moja ni ngozi kukosa hisia unaweza kuungua moto ukachelewa kufahamu, lakini pia ngozi kukosa kuhifadhi mafuta’’,alisema.
Post a Comment