Ni mwezi mmoja umepita baada ya Kampuni ya Apple kutangaza kuwa
watajikita katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, tayari
mshindani wake kibiashara kampuni ya Samsung nao wamepata kibali cha
kutengeneza magari hayo.
Samsung wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo kutoka kwa
Serikali ya Korea Kusini ambako ndiyo makao makuu ya kampuni hiyo
yaliko, huku wakijinadi kuwa wamefikia uamuzi wa kutengeneza magari hayo
kuendana na teknolojia.
Taarifa kutoka mtandao wa Thenextweb zimeeleza kuwa Samsung wataanza kwanza majaribio yao na Kampuni ya magari ya Hyundai na baadae kutengeneza magari yao wenyewe.
“Lengo kubwa la Kampuni yetu ni kuhakikisha dunia inakuwa
salama zaidi sio tu kwa mazingira bali hata viumbe hai ndiyo maana kila
kukicha tunajitahidi kuleta vitu vipya,Teknolojia hii (Magari
yanayojiendesha yenyewe) itasaidia kupunguza msongamano,Kupunguza ajali
na kulinda mazingira“Alisema Afisa mipango wa Kampuni ya Samsung Bw. Young Sohn.
Mwishoni mwa mwaka jana Samsung walinunua kampuni ya HARMAN
inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya ndani vya magari kwa Dola
Bilioni 8 za kimarekani hivyo huenda ilikuwa ni njia ya kujiwekea
urahisi kwa kampuni hiyo kuingia kwenye teknolojia ya magari
yanayojiendesha hivyo tutarajie kuona magari ya kampuni hiyo yenye nguvu
zaidi duniani.
Kwa sasa bei ya magari hayo haijatajwa, kutokana na sababu za kibiashara .
Kampuni ya Samsung itaungana na makampuni mengine makubwa Duniani
kama Tesla, Apple,Google na mengine kibao kwenye ushindani wa soko la
magari yanayojiendesha yenyewe.
Home
»
»Unlabelled
» Soko la magari yanayojiendesha yenyewe lazidi kukua; Samsung nayo ndani
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment