Kumekuwa na utata wa muda mrefu juu ya swala la alama tatu za klabu
ya Simba SC toka kupokwa alama hizo na shirikisho la soka nchini TFF,
swala ambalo klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kariakoo ikisemekana
kusubiria Barua kwa udi na uvumba kutoka Tff ili wapeleke swala hilo
katika ngazi ya Fifa.
Bongo5 imewasiliana na Afisa habari wa TFF ALfredy Lucas ili kuthibitisha juu ya barua hii, na haya ni maneno yake
“Unajua tangu Simba ilivyoanzishwa miaka 80 iliyopita, tumekuwa na
mtindo wa official communication, na Official Communication ni written
barua rasmi, unajua i am wondering kwamba, inaonekana its a big Issue,
kwamba barua barua, ila barua mi nishasema watapewa, na siwezi kusema
wamepewa kumbe wenyewe wakathibitisha hawajapewa, kwa hiyo ni vizuri
zaidi wakathibisha Simba SC kama wamepata ama hawajapata”,.
Alipoulizwa kuhusu barua inayoonekana katika mitandao kama ni ya kweli au La, alikuwa na hili;
“Kwenye hizo Social media ni wao wenyewe wameamua kwa sababu sisi
tumewapelekea wao kama wameamua kuisambaza sidhini kuwa is a big case,
ni taratibu zakawaida, Oficial Communication barua ambayo ilikuwa lazima
wapate, yani sio kwamba walikuwa wanazuiwa wasipate,mi sioni kama
kulikuwa na njia ya kuwazuia wasipate, kwani kwa kitu gani hasa kinacho
zuia wasipate”,.
Na alipoulizwa swali la mwisho kuthibitisha iliyopo ni yenyewe ama sio yenyewe akamalizia kwa kusema.
“Simba waseme wenyewe kama wameshapata msiiamini hiyo ya kwenye media, mimi sitaki kuthibitisha hilo”,.
TFF yaikabidhi Simba barua ya alama tatu
Title: TFF yaikabidhi Simba barua ya alama tatu
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwa na utata wa muda mrefu juu ya swala la alama tatu za klabu ya Simba SC toka kupokwa alama hizo na shirikisho la soka nchini TFF, ...
Post a Comment