Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya Mawaziri
wa Kamisheni ya Pamoja ya Kitaifa kati ya Tanzania na Afrika Kusini,
uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mhe. Mahiga alieleza
mkakati wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini katika kuongeza maeneo
ya ushirikiano hususan katika biashara na uwekezaji.
Waziri
wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Maite
Nkoana - Mashabane akihutubia katika mkutano huo ambao ulitanguliwa na
mkutano wa siku mbili wa Makatibu wakuu. Pamoja na Mambo mengine, Mhe.
Mashabane alieleza umuhimu wa kukuza uhusiano wa kihistoria uliopo baina
ya mataifa hayo mawili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa mataifa
yote. Pia alitumia fursa hiyo kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la
Tanzania kwa kupatwa na msiba ambao umepunguza nguvu kazi na wataalamu
wa kizazi kijacho.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akitoa
utangulizi pamoja na kuratibu ratiba ya ufunguzi wa mkutano.
Sehemu ya Mawaziri wa Tanzania na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakifuatilia Mkutano.
Sehemu nyingine ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini wakifuatilia Mkutano.
Mawaziri
wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Afrika Kusini ambao pia walikua
wenyeviti wa mkutano huo wakitoa ufafanuzi wa ratiba kwa Bi. Mindi
wakati wa mkutano huo wa ngazi ya Mawaziri.
Picha ya Pamoja ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini.
Post a Comment