Msanii wa muziki wa hip hop ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi,
Joseph Haule ‘Professor Jay’ amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa
Tanzania wamekatishwa tamaa ya kuendelea kufanya kazi za sanaa kwa
kukosekana Sheria ya hati miliki.
Rapa huyo amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kikao cha
Bunge na kusema serikali inapaswa kuzingatia kilio hicho cha wasanii kwa
kusimamia kuwepo kwa hati miliki ili kuweza kuongeza pato la taifa
kupitia kazi za wasanii.
“Kilio kikubwa cha wasanii wa Tanzania sasa hivi ni kuhusu masuala
yao ya hati miliki na ukiangalia Sheria ya hati miliki namba 7 ya mwaka
1999 imeonekana kuwa na mapungufu makubwa sana, kiasi kwamba wasanii
watanzania hawapati kile kinachostahili, hawapati jasho lao
linavyotakiwa na wasanii wa Tanzania wamekata tamaa lakini kiukweli
kabisa takwimu na tafiti zilizofanywa na ‘Lulu Art Promoters’ inaonyesha
kwamba wasanii wa Tanzania na sanaa ya muziki pekee yake inachangia
zaidi ya asilimia 1 ya pato la taifa”. Alisema Mbunge huyo
Aidha, Prof. Jay aliendelea kwa kusisitiza kwamba “Muziki ni nyanja
muhimu sana, kiukweli ikitupiwa jicho na kuweza kupewa kipaumbele
wasanii wanaweza wakupata kile kinachostahili ili kuongeza pato kubwa
katika taifa letu.” Alisisitiza Prof. Jay
Professor J apaza sauti kuhusu kilio cha wasanii
Title: Professor J apaza sauti kuhusu kilio cha wasanii
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa hip hop ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi w...
Post a Comment