Vifaa
tiba hivyo ni Vitanda sita vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama
wajawazito,vitanda sita kwa ajili ya kulalia wagonjwa,shuka 12 na viti
sita kwa ajili ya wagonjwa.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema
vimetolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania na vitasaidia katika
kupunguza adha wanayopata akina mama wajawazito wanapofika kupata huduma
katika vituo vya afya.
“Akina
mama ndiyo wanapata adha kubwa wanapohitaji huduma za afya,baada ya
kuona jinsi akina mama hawa wanavyoteseka,niliamua kuanza kutafuta watu
wa kutusaidia,nashukuru ubalozi wa China nchini ulikubali kunipatia
vifaa hivi kwa ajili ya wananchi wa Shinyanga”,alieleza Hamad.
“Vifaa hivi vitasaidia katika kupunguza vifo vya mama na mtoto,naomba mvitunze”,aliongeza Hamad.
Aidha
alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuachana na tabia ya
kuozesha watoto wadogo kwa tamaa ya mali ‘ng’ombe’ kwani takwimu
zinaonesha kuwa watoto wanapopata ujauzito inasababisha wengi wao
kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
“Mkoa
wa Shinyanga tunaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni,naomba tupeleke
watoto shule,waacheni watoto wa kike wasome,wakifeli darasa la saba
watafutieni shughuli ya kufanya siyo kuwaozesha,ni hatari kwa maisha
yao”,aliongeza Hamad.
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu
alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kuzitaja baadhi ya changamoto
katika zahanati,vituo vya afya na hospitali wilayani kuwa ni upungufu
wa watumishi,magari ya wagonjwa na miundo mbinu.
Mwandishi
Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio wakati
mbunge Azza Hilal Hamad akiwa wilayani Kishapu kukabidhi vifaa tiba
pamoja na kuzungumza na wananchi
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad Jumamosi
Mei 6,2017 amekabidhi Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 12.6 katika vituo vya afya vinne vya afya ambavyo ni
Nhobola,Songwa,Ng’wang’haranga na Dulisi vilivyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Hapa ni ndani ya kituo cha afya Nhobola wilayani Kishapu-Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (wa pili
kushoto) akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola
kilichopo kata ya Talaga,Bhujiku Mganga Nyanda
Mganga
mkuu wa Kituo cha afya Nhobola Bhujiku Mganga Nyanda akieleza jinsi
akina mama wajawazito walivyokuwa wanapata changamoto wakati wa kupata
matibabu
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akiwa katika wodi ya wazazi amebeba mtoto wa mkazi wa Kata ya Talaga
baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Nhobola
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akifurahia kubeba mtoto mwingine aliyezaliwa katika kituo cha afya
Nhobola
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF)
akimkaribisha Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza
Hilal Hamad (CCM) katika mkutano wa kukabidhi vifaa tiba katika kituo
cha afya Nhobola
Katibu
wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akizungumza katika kituo cha
afya Nhobola kabla mbunge Azza Hamad kuendesha zoezi la kukabidhi vifaa
tiba
Kaimu katibu Umoja wa Akina mama wa CCM mkoa wa Shinyanga Rhoda John akizungumza katika kituo cha afya Nhobola
Mganga
mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akielezea
changamoto zilizopo katika vituo vya afya,zahanati na hospitali wilayani
Kishapu
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF)
akifungua mkutano wa mbunge Azza Hilal Hamad katika kituo cha afya
Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nhobola Mohammed Shamte (Chama cha Wananchi- CUF)
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akielezea kuhusu msaada wa vitanda vya kujifungulia,kulalia na viti vya
wagonjwa katika kituo cha afya Nhobola
Vitanda
vitatu vya kulalia wagonjwa,kitanda kimoja cha kujifungulia na viti vya
wagonjwa vilivyotolewa katika kituo cha afya Nhobola
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kisasa cha kujifungulia
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha kitanda cha kulalia wagonjwa
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akionesha shuka zitakazotumika katika vitanda alivyopeleka katika kituo
cha afya Nhobola
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa viongozi wa kijiji,kata na
wilaya ya Kishapu
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa kata ya Talaga
Diwani
wa kata ya Talaga Richard Kazangu Dominiko( CCM) akitoa neno la
shukrani baada ya mbunge Azza Hilal Hamad kukabidhi vifaa tiba katika
kituo cha afya Nhobola
Mkazi
wa kijiji cha Nhobola aliyejulikana kwa jina la Ng'wani Sali
akimshukuru mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza
Hilal Hamad (CCM) kupeleka vitanda katika kituo cha afya Nhobola
Hapa ni katika kata ya Songwa-Pichani
wakazi wa kata ya Songwa wilayani Kishapu wakijiandaa kumpokea Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) alipowasili
katika kata ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo
vitanda,shuka na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
Wananchi
waliobeba matawi ya miti wakiwa wamemzingira Mbunge wa Viti Maalum mkoa
wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) alipowasili katika kata
ya Songwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda,shuka na
viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Songwa
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akiwa amefungwa nguo huku akiandamana na wananchi kuelekea eneo la
mkutano wa hadhara katika kata ya Songwa
Wananchi waliobeba matawi ya miti wakiandamana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
Maandamano kuelekea eneo la mkutano yakiendelea
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akifurahia na wananchi waliompokea
Kikundi
cha ngoma za asili kikitumbuiza baada ya mgeni rasmi mheshimiwa Azza
Hilal Hamad kufika eneo la mkutano kabla ya kukabidhi vifaa tiba katika
kituo cha afya Songwa
Wacheza ngoma wakisalimiana na Mbunge Azza Hilal Hamad (CCM)
Wacheza ngoma ya asili 'Wanunguli' wakitoa burudani
Mcheza ngoma ya Ununguli akimshika nyoka
Mcheza ngoma ya Ununguli akiwa amemkamata nyoka
Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Hellena Chacha akiwasalimia wananchi wa kata ya Songwa
Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akiteta jambo la mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akicheza wakati kwaya ya AICT ikiimba wimbo wa amani ambao ulimfurahisha
na kuwaahidi kuwadhamini ili waurekodi wimbo huo
Akina mama wakiimba shairi
Diwani wa kata ya Songwa Abdul Mohammed Ngolomole akizungumza wakati wa mkutano wa mbunge Azza Hilal
Suzana Yohana akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa kata ya Songwa
Mzee
Hamis Bulege akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge
Azza Hilal Hamad,zawadi iliyotolewa na wazee wa Songwa ikiwa ni ishara
ya kuwa wanamkubali kama kiongozi mzuri anayejali wananchi wake
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akipokea zawadi ya mbuzi
Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt. Josephat Shani Mudamu akizungumza
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa kata ya Songwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizunguza
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akisitiza jambo
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi
vitanda vya kulalia na kitanda cha kujifungulia pamoja na viti vya
wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad akionesha shuka zilizotolewa katika kituo cha afya Songwa
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad
akizungumza baada ya kukabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Songwa.
Post a Comment