|
Tunisia
imesema Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) ni
lazima itangazwe kwa nguvu zote ili kuwawezesha wananchi barani Afrika
kufahamu uwepo wake,malengo ya kuanzishwa kwake pamoja na shughuli zake.
Akipokea
ujumbe wa Mahakama hiyo katika Ikulu ya Tunisia,Rais wa Nchi Hiyo
,Mh.Beji Caid Essebsi alipongeza uanzishwaji wa Mahakama hiyo na
kuongeza kuwa inahakikisha ulinzi wa Haki za Binadamu Barani
Afrika.
“Kwa
njia hii,Haki za Binadamu Barani Afrika zitalindwa na kuhakikisha
maendeleo endelevu ya demokrasia kwa wananchi” Aliuambia ujumbe huo
uliohusisha majaji watatu akiwemo Rais wa AfCHPR,Jaji Sylvain Ore’.
Kwa
upande wake Rais wa AfCHPR, Jaji Ore’ aliishukuru serikali ya Tunisia
kwa kukubali kuupokea ujumbe wake na kukutana na Viongozi na Maafisa
mbalimbali wa nchi hiyo na pia kuendesha semina kwa wadau mbalimbali
nchini humo kwa lengo la kuitangaza Mahakama.
Wakati
wa ziara hiyo,Tunisia ilitia saini tamko la kuruhusu watu binafsi na
Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s) katika nchi hiyo kupeleka kesi zao
moja kwa moja katika Mahakama hiyo yenye Makao yake makuu Jijini
Arusha.
Hatua
hiyo ya Tunisia ambayo ni utekelezaji wa kifungu cha 34(6),Inalifanya
Taifa hilo kuwa Nchi ya nane Barani Afrika kukubali makundi hayo
kupeleka kesi katika Mamlaka za Mahakama hiyo.
Nchi
nyingine ambazo ni Wanachama wa umoja wa Afrika zilizotoa tamko
kukubali Watu binafsi na NGO’s kutoka katika Nchi zao kupeleka kesi
katika AfCHPR ni pamoja na:Benin,Burkina Faso,Côte
d’Ivoire,Ghana,Malawi,Mali na Tanzania.
Utiwaji
saini wa tamko hilo ulifanywa na Waziri wa mashauri ya kigeni wa
Tunisia,Mh.Khemaies Jhinaoui kwa niaba ya Serikali ya Nchi yake.
Rwanda
ambayo hapo awali ilitia saini kukubali tamko hilo sasa imejitoa ingawa
Mkutano wa Kilele wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis
Ababa,Ethiopia mapema mwaka huu uliitaka nchi hiyo kutafakari juu ya
uamuzi wake huo.
Kwa
upande wake Misri ambayo haijaridhia itifaki iliyoanzisha Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilieleza kuridhishwa kwake na
utekelezaji wa shughuli za Mahakama hiyo katika kipindi cha miaka 10
iliyopita na kuahidi kuwa itaridhia itifaki husika.
Mahakama
hiyo ilifanya ziara ya kikazi Nchini Tunisia na Misri kuanzia April 9
hadi 14 Mwaka huu kwa lengo la kukuza uelewa wa wadau mbalimbali juu ya
uwepo ya Mahakama,Malengo yake na shughuli zake.
Tangu
mwaka 2010,AfCHPR imefanikiwa kuendesha ziara 27 za kuelimisha katika
Maeneo mbalimbali Barani Afrika na kuendesha Semina na Mikutano ili
kukuza uelewa wa Masuala kuhusu ulinzi wa Haki za Binadamu Barani humo
na kuhamasisha Nchi wanachama wa AU kuridhia mkataba ulioanzisha
Mahakama hiyo na kutoa tamko la kuruhusu watu binafsi na NGO’s kupeleka
kesi zao Mahakamani hapo.
AfCHPR
ilianzishwa na Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika(AU) kwa mujibu wa
kifungu namba 1 cha itifaki ya Mkataba ya Mahakama hiyo na ilianza
shughuli zake rasmi Novemba,2006 kwa lengo la kuimarisha Haki za
Binadamu na Watu Barani Afrika.
Post a Comment