Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Taarifa muhimu kuhusu Hisa za Vodacom Tanzania
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom (VTL). Kwa mfano, ujumbe uliosambaz...

Kumekuwa na taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom (VTL). Kwa mfano, ujumbe uliosambazwa tarehe 19 Aprili umedai kuwa bei ya TZS 850 kwa hisa ni mara 3.8 zaidi ya thamani halisi ya hisa hizi. Kufikia hapo, mwandishi alikokotoa thamani ya vitabuni ya rasilimali za kampuni, akatoa dhima (madeni), na kudai kuwa albaki ndiyo thamani halisi ya hisa za wamiliki wote wa kampuni. Njia hii ni potofu, na inaonyesha ni kwa kiwango gani mwandishi haelewi jinsi thamani za hisa na kampuni zinavyo kokotolewa. Kwa mfano, mwandishi anadai kuwa ukweli kwamba bei ya toleo ya hisa za VTL ya TZS 850, sawa na mara 3.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali kujitoa dhima, ni ushahidi kuwa bei imewekwa ya juu sana. Lakini siku hiyo hiyo, bei ya hisa za Safaricom katika siko la hisa la Nairobi ilikuwa ni mara 5.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali baada ya kutoa dhima.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top