Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na wapenzi wake
kuwa imesitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne wiki ijayo
25.04.2017, baada ya nia na dhamira njema ya serikali kutaka
kushughulikia sintofahamu inayoendelea baina ya klabu na Shirikisho la
Soka nchini (TFF).
Ikumbukwe jana klabu yetu, ililiandikia barua Jeshi la Polisi nchini
ikiomba kibali cha kufanya maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa
na viongozi, wanachama na washabiki wa klabu yetu kwenda Wizara
inayosimamia Michezo nchini, yakiwa na lengo la kupeleka kilio chetu juu
ya namna TFF inavyoshughulikia malalamiko ya muda mrefu na ya sasa ya
klabu hii kubwa nchini.
Katika barua iliyoandikwa na katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) Mohammed Kiganja kwa niaba ya Serikali, imetutaka Shirikisho
na Klabu kutafuta namna sahihi na iliyo na weledi katika kushughulikia
changamoto hizi zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
Serikali kupitia barua hiyo, imeahidi pia kutukutanisha pande zote
haraka iwezekanavyo, ili kwa pamoja tumalize sintofahamu hii kwa maslahi
ya mchezo wa mpira wa miguu Tanzania.
Klabu ya Simba inachukua nafasi hii ya kipekee kuishukuru serekali
kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa hatua mahsusi na za haraka
katika kutafuta suluhisho la kudumu la jambo hili.
Tunawaomba wanachama na washabiki wetu watulie na sote tuache
majibizano yoyote ili kutoa fursa kwa Serikali kusimamia kikamilifu
jambo hili.
Klabu ya Simba inafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi nchini kuwajulisha kusudio letu la kusitisha maandamano hayo.
IMETOLEWA NA…
Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba SC
Simba nguvu moja
Simba imesitisha maandamano ya amani
Title: Simba imesitisha maandamano ya amani
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na wapenzi wake kuwa imesitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne wiki ijayo 25.04.2...
Post a Comment