Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao
kipo tayari kupambana na timu yoyote katika mchezo wa nusu fainali ya
kombe la FA au Azam Sports Federation Cup huku akiamini watafanya vizuri
na kusonga mbele kucheza fainali ya michuano hiyo.
Tayari timu nne zinazotarajiwa kucheza nusu fainali zimeshajulikana
(Simba, Mbao FC, Azam FC na Yanga) ambazo zitambana kutafuta washindi
wawili watakaocheza fainali.
“Yoyote atakaepangwa na sisi kwenye hatua ya nusu fainali tutapambana
nae ili kupata ushindi na kufika hatua ya fainali. Hata tukipangwa na
Simba ndio tayari ratiba itakuwa inaonesha hivyo, tupo tayari kuwakabili
kwa sababu huwezi kuwa bingwa bila kukutana na mpinzani wako, lazima
umshinde ndipo uchukue kombe.”
Yanga walipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye
mchezo uliochezwa jana April 22, 2017 na kufanikiwa kusonga mbele
kwenye hatua hiyo ya nusu fainali.
Droo ya kuzipata timu zitakazo pambana kwenye nusu fainali
itachezeshwa leo kwenye ofisi za Azam TV ambao ndiyo wadhamini wakuu wa
michuano hiyo ambayo msimu huu ilishirikisha jumla ya timu 86 (ligi kuu
timu 16, ligi daraja la kwanza timu 24 na ligi daraja la pili timu 24)
‘Hata tukikutana na Simba poa tu’ Cannavaro
Title: ‘Hata tukikutana na Simba poa tu’ Cannavaro
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao kipo tayari kupambana na timu yoyote katika mchezo wa nusu fainali ya komb...
Post a Comment