Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akitoa chanjo kwa mtoto wa umri wa
siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo
katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi
ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya
Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo
Mkoani Singida.
Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akifurahi mara baada ya kutoa chanjo
kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani
Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi
ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya
Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo
Mkoani Singida.
Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani
Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
………………………………………………………………………
Wazazi
wanaoshindwa kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki
za binadamu hasa haki ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za
serikali za kupambana na maradhi, umaskini na ujinga.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake
iliyosomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo
wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika
hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida.
Dkt.
Nchimbi amesema watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano
wanapaswa kupata chanjo zote ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini,
surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, na pepopunda ambayo yanazuilika kwa
chanjo na motto akiugua kupona ni nadra
“Mtoto
akiumwa magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona
anaweza kupata ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie
kukamilisha chanjo zote” amesisita
Ameongeza
kuwa serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote
zinapatikana na hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha
motto anapata chanjo pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale
wasiowapeleka watoto kupata chanjo.
Akisoma
taarifa ya hali ya chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Salum
Manyatta amesema Mkoa wa Singida kwa sasa una chanjo zote zinazohitaji
na zinatolewa katika vituo 197 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi
na moja jioni.
Dkt.
Manyatta amesema kwa mkoa wa Singida wananchi wana uelewa wa chanjo
ambapo kila mwaka zaidi ya asilimia 95 hufikiwa na chanjo karibia zote
huku changamoto ikiwa ni katika kukamilisha chanjo ambazo huhitaji dozi
zaaidi ya moja.
Ameongeza
kuwa baadhi ya wazazi hujifungulia nje ya vituo vya kutolea huduma za
afya mfano majumbani na hivyo kupelekea watoto kukosa chanjo za awali.
Dkt.
Manyatta amesema katika kukabiliana na changamoto za baadhi ya watoto
kukosa chanjo, jitihada zilizowekwa ni pamoja na kupitia kadi ya mtoto
kuona endapo amekamilisha chanjo kabla hajapewa huduma nyingine za afya.
Jitihada
nyingine ni viongozi wa serikali ngazi za vijiji kuandaa orodha ya
watoto ambao hawajakamilisha chanjo na kuwafatilia wazazi au walezi
wakamilishe chanjo hizo, kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa chanjo
na kutoa huduma ya mkoba na kliniki tembezi ili kuwafikia watoto
wanaoishi maeneo ya vijijini sana.
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo mwaka huu ni “Chanjo Humkinga Kila Mtu, Pata Chanjo”.
Post a Comment