Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe
kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, iliyowasilishwa kwake na
Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias
Malimba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na
Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es
salaam, Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa
Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze
Rais amepokea barua hiyo, Alhamisi Ikulu, kutoka kwa mjumbe maalum
akiwa ni waziri wa Elimu Rwanda Dkt Malimba, aliiwasilisha kwa Rais
Magufuli.
Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa pamoja na kupokea barua hiyo,
Mheshimiwa Rais Magufuli na Dkt Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali
ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu
hususan maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya
Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania
ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.
Rais Magufuli kupeleka walimu wa Kiswahili Rwanda
Title: Rais Magufuli kupeleka walimu wa Kiswahili Rwanda
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, iliyowasilishwa kwake na Mjum...
Post a Comment